Na Shaffih
Dauda
KOCHA wa Timu
ya taifa ya Tanzania, Mholanzi, Mart Nooij aliamua kuwaanzisha washambuliaji
wanne katika mechi dhidi ya Msumbuji, kuwania kupangwa hatua ya makundi ya kusaka
tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika, AFCON, mwakani nchini Morroco.
Mbwana Ally
Samatta, Thomas Ulimwengu, John Bocco `Adebayor` na Mrisho Ngassa, wote kwa
pamoja walianza katika sare ya 2-2 ndani ya uwanja wa Taifa, jinini Dar es
salaam dhidi ya `Black Mambas`.
Lengo la
Nooij lilikuwa ni kushambulia kwa nguvu ili kupata mtaji mkubwa wa mabao kabla
ya mechi ya marudiano itakayopigwa wiki mbili zijazo mjini Maputo nchini
Msumbiji.
Lakini kwa
mtazamo wangu, niliona mapungufu juu ya namna kocha Nooij alivyowapanga
washambuliaji hawa. Ulimwengu na Ngassa walicheza pembeni, Samatta na Bocco
walisimama katikati.
Mimi naona
ingekuwa na tija kama Thomas angecheza katikati kuliko kucheza pembeni ili
kupata ubora wa timu.
Kwa timu
ilivyoanza yeye alikuwa kulia, katikati alikuwa Mbwana Samatta na John Bocco,
kushoto alicheza Mrisho Ngassa na wakawa wanabadilishana.
Lakini mimi
naona ingekuwa na tija zaidi kama Thomas Ulimwengu angesimama katikati na John
Bocco, halafu samata akawa anashambulia kutoka pembeni upande wa kushoto,
halafu Mrisho Ngassa ashambulie kutoka kulia. Kwasababu kwa aina ya uchezaji wa
Ulimwengu, walipokuwa wanamuweka pembeni walikuwa wanampatia ugumu.
Alikuwa
analazimika apige chenga, apige pasi kutoka eneo alipo, lakini yeye sio aina ya
mchezaji wa hivyo vitu, yeye sio mtu wa vitu, yeye ni mtu wa kuwekewa mpira ili
awe na chaguo moja tu, kupiga au kupasia
karibia na goli ili kumpa mwenzie afunge, na hapo unaweza kuona ubora wa Thomas
Ulimwengu.
Kama
Ulimwengu angekuwa katikati ingekuwa ni vizuri zaidi kucheza mipira mirefu waliyokuwa
wanacheza akina `Cannavaro` dakika za kipindi cha kwanza. Mara nyingi mipira
hii mabeki wa Msumbiji walikuwa wanaicheza, kwasababu John Bocco pamoja na umbile kubwa, mrefu, lakini sio mzuri
kupambana, ni mwepesi, kwahiyo ni mara mia nane angekuwepo Thomas Ulimwengu,
kwasababu ni mtu mwenye nguvu na jinsi mwili wake ulivyo angeweza kupambana nao
na kutoa mianya kwa akina Ngassa, Samatta au Bocco mwenyewe kufungwa.
Hii ni
kwasababu mabeki wa Msumbiji
wangelazimika kuokoa mipira hovyo, na ingedondoka maeneo ambayo wengine wangeokota
baada ya mikikimikiki ya Ulimwengu.
Halafu
kingine, ile mipira, Ulimwengu angekimbia nayo katoka katikati na kutanua kwenda
pembeni. Hii ingetoa nafasi kwa akina Ngassa au Samatta kutegemeana mpira
unaenda upande upi.
Mabeki wangelazamika
kwenda kukimbiza na kuacha nafasi katikati, na kwasababu yeye ana kasi angewahi
ile mipira na kupiga krosi ambazo zingeweza kufungwa na wenzake kwasababu katikati pale pangeachwa wazi kutokana
na mebeki kwenda pembeni kumkimbiza Ulimwengu.
Lakini ilikuwa
ni ngumu kwa Ulimwengu kutokea pembeni na kupiga mipira vizuri kwasababu yeye
hana uwezo wa kumiliki mpira vizuri, sio mtu wa kuchezea mpira kama akina
Ngassa au Samatta mwenyewe.
Unajua
Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta, John Bocco wote ni washambuliaji wa kati, lakini
wanatofautiana ujuzi na aina ya
uchezaji.
Kama mimi
ningekuwa kocha na ningetaka kuwatumia wote kwa wakati mmoja, mara mia nane,
huyu Thomas Ulimwengu angesimama katikati, halafu Jonh Bocco au Samatta angeenda
pembeni.
Lakini mimi
ningependa zaidi Mbwana Samatta atokee pembeni upande wa kushoto, kwasababu ana
uwezo, ana kasi, na anaweza kupiga chenga na kutafuta `engo` ya kupiga mpira.
Anaweza kupiga chenga, akarudi na kuuzungusha.
Kuthibitisha
pointi yangu hiyo, kuna wakati Samatta alikwenda pembeni, alipiga pasi mbili
ambazo almanusura zisababishe goli. Alipiga krosi moja ambayo alipigwa kichwa
na John Bocco, lakini kipa akacheza.
Akapiga krosi
nyingine ambayo beki alitoa ikawa kona. Kwahiyo, kwayeye kucheza pembeni ilikuwa na faida zaidi
kuliko Thomas Ulimwengu.
Chanzo: shaffihdauda.com
0 comments:
Post a Comment