Kocha mkuu wa Ruvu Shooting, Mkenya Tom Alex Olaba amewaamini vijana wake chini ya umri miaka 20
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Julai 25, 2014, saa 3:23 asubuhi
KOCHA mkuu wa Ruvu Shooting, Mkenya Tom Alex Olaba
amedhamiria kukijenga upya kikosi chake kwa kuwapa uzoefu vijana wenye umri
chini ya miaka ishirini (U-20) waliowapandisha kutoka timu B na wale
waliosajiliwa wakati wa majaribio.
Ruvu Shooting aliwafanyia majaribio wachezaji
vijana kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania mwezi mei mwaka huu na wale
waliofuzu walijiunga na timu B.
Ikiwa ni sehemu ya kuwaimarisha na kuwapa uzoefu
wa kucheza ligi kuu, Olaba anawapa nafasi ya kucheza mechi mbalimbali za
kirafiki.
Kocha huyo aliyefungwa bao 1-0 na Azam jana katika
uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini Dar es salaam alisema vijana wake
hawajapata uzoefu, lakini wanaonekana kucheza vizuri na kadiri siku
zinavyokwenda hofu inawatoka.
“Ukiangalia jinsi tulivyocheza mechi ya kirafiki
na Azam fc, utagundua haraka haraka kuwa vijana wa U-20 walikuwa na wasiwasi,”.
Alisema Olaba.
Msimi uliopita, Ruvu Shooting walifungwa mabao 7-0 dhidi ya Yanga sc uwanja wa Taifa
“Kipindi cha kwanza tulicheza vizuri sana, lakini
kipindi cha pili wao wakapata goli moja. Kufungwa kwangu, mimi sina neno. Nina maana yangu ya kucheza ya
mechi za kirafiki”.
“Niliwaweka U-20, ndio mara yao ya kwanza kucheza
na Azam, ukiwatazama unaona walitetemeka. Azam wengi wao ni wachezaji wa
kigeni, wachezaji wangu wa U-20 wamepata uzoefu mkubwa. Aliongeza Olaba.
Aidha, Olaba alisema kuwa anatarajia kucheza mechi
nyingi zaidi za kujipima uwezo baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, lengo
likiwa ni kukisuka kikosi kwa ajili ya ligi kuu inayotarajia kuanza kushika
kasi septemba 20 mwaka huu..
“Nitacheza mechi nyingi sana, hata hivi leo ninacheza na JKT Ruvu Stars hapa kwetu
Mabatini. Baada ya sikuu ya ramadhani nitacheza mechi nyingi sana, siwezi
kutaja idadi”. Aliongeza Olaba.
“Kila kocha anapocheza mechi za kirafiki anaona
makosa, akirudi nyumbani anaenda kurekebisha”.
Msimu uliopita, Olaba aliyerithi mikoba ya
aliyekuwa kocha mkuu na akatimkia Yanga sc, Charles Boniface Mkwasa `Master` aliiongoza Ruvu Shooting kushika nafasi ya 6 katika
msimamo wa ligi kuu kwa kujikusanyia pointi 38 kibindoni.
Walishinda mechi 10, walitoka sare mechi 8 na
kufungwa mechi 8. Idadi ya mabao waliyofunga yalikuwa 28 na walifungwa mabao
32.
0 comments:
Post a Comment