Imechapishwa Julai 21, 2014, saa 10:30 jioni
MANCHESTER United wiki hii wapo tayari kuanza
kuifukuzia saini ya kiungo wa Juventus, Arturo Vidal kwa dau la Euro milioni
54.
Klabu hiyo ya Old Trafford imejiamini kuwa
itamnasa nyota huyo wa Chile katika fainali za kombe la dunia na wanaanza
harakati zaidi kumuwinda kiungo huyo
mwenye miaka 27.
Louis Van Gaal ambaye alitambulishwa rasmi kuanza
kazi jumatano ya wiki iliyopita, ni shabiki mkubwa wa Vidal na aliwahi kujaribu
kumsajili alipokuwa anafanya kazi Bayern Munich mwaka 2011 na amethibitisha
kumhijtaji tena.
Mholanzi huyo alijaribu kumshawishi Vidal mapema
mwezi Julai, licha ya klabu yake kuambiwa kuwa itawagharimu Euro milioni 56
jumlisha Luis Nani.
Juventus wamemsajili Alvaro Morata kutoka Real
Madrid na wanapambana kumnasa Roberto Pereyra, wakati huo huo inapendekezwa
kuwa Vidal auzwe ili kupata hela.
Vidal ambaye kwasasa anapumzika nchini Chile kufuatia
kumalizika kwa fainali za kombe la dunia, hivi karibuni alisema hatima yake
Turin ipo mashakani.
“Sidhani kama muda wangu Juventus umekwisha,
ingawa siwezi kusema kwasasa,” aliiambia Radio ya Chile. “Nitakaporudi kutoka
Chile, nitazungumza na mabosi wangu na tutaona kitakachotokea”.
Mkurugenzi wa Juve, Pavel Nedved alisema klabu
inaona ugumu kuwauza Vidal na Pogba, lakini alikiri dau kubwa linaweza
kuwalazimisha kufanya biashara.
‘Mipango yetu ipo wazi, tunataka kuwabakisha
wachezaji wote muhimu wakiwemo Vidal na Pogba,” . Aliwaambia Tuttospot. “Hatudhani kama tutauza
mchezaji yeyote hususani Vidal”.
‘Lakini kama kuna dau kubwa, tunaweza kulifikria
hilo, lakini hatutaki kuuza mabingwa wetu”.
0 comments:
Post a Comment