Imechapishwa Julai 24, 2014, saa 2:38 usiku
LAURENT Blanc amegoma kuweka wazi kama Paris
Saint-Germain imefanya mazungumzo juu ya kumsajili nyota wa Real Madrid, Angel
Di Maria.
Di Maria alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha
Carlo Ancelotti kilichotwaa ubingwa wa UEFA msimu uliopita, lakini hatima yake
ya baadaye imekuwa shakani baada ya usajili wa Toni Kroos na James Rodriguez.
Bosi wa Manchester United, Louis Van Gaal
anavutiwa na mchezaji huyo mwenye miaka 26 na mashetani wakundu walifikia
makubaliano binafsi mapema majira haya ya kiangazi mwaka huu.
Lakini PSG wamekuwa mstari wa mbele kutaka
kumsajili nyota huyo kutokana na jeuri yao ya fedha na Rais wa klabu hiyo
Nasser AL-Khelaifi aliripotiwa kufanya mazungumzo mjini Madrid.
Alipoulizwa juu ya usajili wa Di Maria, Blanc
alisema; “Nawaacha mfuatilie, kwasasa hakuna chochote kilichofanyika”.
0 comments:
Post a Comment