Ombi jipya: Arsenal wanataka kumsajili kiungo wa William Carvalho.
Imechapishwa Julai 21, 2014, saa 7:20 mchana
ASERNAL wametuma maombi ya kutaka kumsajili kiungo wa Sporting Lisbon, William Carvalho mwenye thamani ya paundi milioni 35.
Washika bunduki wapo katika harakati za kutaka kusajili kiungo wa Ulinzi na wanaiwinda saini ya kinda huyo mwenye miaka 22.
Ingawa inafahamika kuwa Sporting wanahitaji ofa ya paundi milioni 35.6 ili kuvunja mkataba wake.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno, aliichezea timu yake ya taifa kwa dakika 90 katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kwenye fainali za kombe la dunia nchini Brazil.
kwa muda mrefu sasa amekuwa akihusishwa kujiunga na Manchester United na sasa Asernal wameingia vitani.
Wakati huo huo , washika bunduki wa London wamekubali kulipa paundi milioni 3.2 kama ada ya uhamisho ya kipa wa Nice David Ospina.
Kipa huyo mwenye miaka 25 alifanya vizuri akiwa na Colombia katika mechi za kombe la dunia na ataleta ushindani kwa kipa wa sasa, Wojciech Szczesny.
Dau limekubaliwa: Arsenal wanatarajia kumsajili kipa wa Colombia David Opsina kutoka kutoka klabu ya Nice ya Ufaransa.
0 comments:
Post a Comment