Na Boniface Wambura, Johannesburg
Imechapishwa Julai 31, 2014, saa 7:47 mchana
Kikosi cha Taifa Stars kimewasili salama jana (Julai 30 mwaka
huu) hapa Johannesburg kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya kwenda
Maputo, Msumbiji kwa ajili ya mechi dhidi ya Mambas itakayochezwa Jumapili.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefanya
mazoezi mara mbili leo- asubuhi na jioni kwenye uwanja wa Bedfordview Country
Club. Mazoezi ya mwisho yatafanyika kesho asubuhi (Agosti 1 mwaka huu) kabla ya
baadaye jioni kuanza safari ya Maputo.
Wakati huo huo, Balozi wa Tanzania hapa Afrika Kusini, Razia
Msuya baadaye leo jioni atazitembelea timu zote mbili za Tanzania zilizopo hapa
Johannesburg kusalimia wachezaji.
Serengeti Boys yenyewe ipo hapa tangu Julai 27 kwa ajili ya
mechi dhidi ya Afrika Kusini itakayochezwa Jumamosi (Agosti 2 mwaka huu).
0 comments:
Post a Comment