TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars chini ya
kocha mkuu, Mholanzi, Mart Nooij imelazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya
Msumbiji `Black Mambas` katika mchezo wa kuwania kupangwa hatua ya makundi
kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya mataifa ya Afrika, AFCON, mwakani nchini
Morocco.
Msumbiji walipata penati katika dakika ya 47 iliyozamishwa
nyavuni na mshambuliaji tegemeo, Elias Gasper Pelembe.
Dakika ya 65 Khamis Mcha `Vialli` aliyetokea benchi
na kuchukua nafasi ya Mrisho Ngassa,
aliunganisha krosi iliyochongwa na Shomary Kapombe na kuisawazishia Stars bao
hilo.
Dakika 6 baadaye, Stars ilipata penati na Mcha
akafungga bao la pili na la kuongoza.
Dakika za lala salama, Stars walifanya shambulizi
kali ambapo mpira uliopigwa na Thomas Ulimwengu uligonga mwamba, lakini
Msumbiji walitumia muda huo kufanya shambulizi la kushitukiza na kufunga bao la
kusawazisha katika dakika ya 87 kupitia kwa Isaac Carvalho.
Bao hilo lilitokana na wachezaji wa Taifa stars
kujisahau na Mambas wakatumia muda huo kuwaadhibu.
Kwa matokeo hayo, Stars inahitaji ushindi wa aina
yoyote ugenini au kutoka sare ya mabao 3-3 ili kufuzu hatua ya makundi.
0 comments:
Post a Comment