Imechapishwa Julai 30, 2014, saa 12;42 jioni
TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars chini ya
kocha mkuu, Mholanzi Mart Nooij imeondoka jioni ya leo kwa ndege ya Air
Tanzania kuelekea nchini Afrika kusini itakapoweka kambi ya siku mbili kabla ya
kwenda mjini Maputo kucheza mechi ya marudiano dhidi ya Msumbiji.
Taifa Stars iliwasili leo asubuhi kwa ndege ya
Fastjet kutoka kambini mjini Tukuyu, mkoani Mbeya na kuunganisha safari ya
Afrika kusini jioni.
Mechi hiyo ya marudiano itapigwa agosti 3 mwaka
huu uwanja wa Taifa wa Zimpeto uliopo
nje kidogo ya jiji la Maputo.
Gereda, Thomas Ulimwengu ataungana na Taifa Stars nchini Afrika kusini
Katika mchezo wa kwanza, Taifa Stars ilitoka sare ya mabao 2-2 na ‘Black Mambas’ ndani ya dimba la Taifa jijini Dar es salaam Julai 20 mwaka huu.
Katika mchezo wa kwanza, Taifa Stars ilitoka sare ya mabao 2-2 na ‘Black Mambas’ ndani ya dimba la Taifa jijini Dar es salaam Julai 20 mwaka huu.
Taifa Stars wanahitaji ushindi wa aina yoyote au
sare ya mabao 3-3 au zaidi ili kusonga mbele hatua ya makundi ya kuwania kusaka
tiketi ya kushiriki fainali za mataifa ya Afrika, AFCON mwakani nchini Morocco.
Wachezaji wa kimataifa wa Tanzania wanaocheza TP
Mazembe, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu watajiunga na wenzao nchini Afrika
kusini leo wakitokea Mjini Lubumbashi nchini DR. Congo.
Wakati Mwinyi Kazimoto anayecheza soka la kulipwa
nchini Qatar tayari alitua nchini na leo hii ameondoka na timu.
0 comments:
Post a Comment