Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Julai 31, 2014, saa 1:20 usiku
KLABU ya Simba sc imemalizana na
klabu ya Ruvu Shooting kuhusu kumsajili mshambuliaji wa maafande hao, Elias
Maguri .
Afisa habari wa klabu hiyo, Masau
Bwire amesema wakati wa sikuu ya Eid El Fitri, Simba walipeleka ofa, wakakaa pamoja
na kujadili na hatimaye kufikia makubaliano.
“Simba wamefuata taratibu zote,
wamekuja kwetu, kwasababu Maguri ana
mkataba na sisi. Tumekubaliana na kilichobaki ni mchezaji mwenyewe kumalizana
na Simba kwa maslahi binafsi,” alisema Masau.
Masau aliongeza kuwa kwasasa Maguri
yupo kambini Ruvu Shooting na anasubiriwa na Simba ili wakafikie makubaliano
binafsi ili asaini mkataba.
Maguri ni miongoni mwa washambuliaji
waliokuwepo katika mipango ya kocha mkuu wa Simba, Mcroatia, Zdravko Logarusic.
Awali Ruvu Shooting waliwashutumu
Simba kutaka kufanya usajili wa kinyemela na kuwataka wafuate taratibu zote
zinazotakiwa kwasababu wao wana haki zote za mchezaji.
Simba walifyata mkia na kuwafuata
Shooting ambapo sasa wamefikia makubaliano baina ya pande zote mbili. Hata hivyo
ada ya uhamisho ya Maguri haijawekwa wazi.
0 comments:
Post a Comment