Waziri wa Habari,
vijana, utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara (katikati) alipokutana na
kamati ya maandalizi ya ziara ya magwiji wa Real Madrid nchini leo ofisini
kwake jijini Dar es salaam
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
SERIKALI imeahidi kutoa ushirikiano wa kutosha
wakati wa ziara ya magwiji wa Real Madrid maarufu kama ‘Real Madrid Legends’
wanaotarajia kutua nchini Agosti 22 mwaka huu na kucheza mechi moja ya kirafiki
dhidi ya kikosi maalumu cha nyota wa Tanzania.
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa habari, vijana,
utamaduni na michezo, Dkt. Fenella Mukangara alipotembelewa na kamati ya
maandalizi ya ziara hiyo katika ofisi yake katikati ya jiji la Dar es salaam.
Lengo la kamati hiyo chini ya mwenyekiti
wake, Farough Baghozah kumtembelea
waziri ilikuwa ni kumueleza rasmi juu ya tukio hilo kubwa la kihistoria.
Wiki iliyopita, kamati hiyo ilimtembelea mkuu wa
mkoa wa Dar es salaam, Saidy Mecky Sadick
na kumjulisha ujio wa magwiji hao ambapo kwa upande wake alifurahishwa na tukio
hilo na kusema Dar es salaam ipo tayari kuwapokea.
Sadick aliahidi kutoka ushirikiano mkubwa ikiwemo
kuhakikisha suala la ulinzi na usalama kwa wakati wote ambao magwiji hao watakuwepo
jijini Dar es salaam linaimarisha kwa kiwango cha juu.
Meneja wa ziara hiyo, Dennis Ssebo amesema
wamepokelewa vizuri na Dkt. Fenella ofisini kwake na amesema serikali
itashirikiana kwa ukaribu ili kufanikisha suala hilo.
“Tumekaribishwa vizuri na mheshimiwa Dkt. Fenella
na amesema serikali inalipokea kwa mikono miwili tukio hili kubwa na la
kihistoria”. Alisema Ssebo.
Mbali na kucheza mechi ya kirafiki Agosti 23 mwaka
huu, magwiji hao watapata fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii
nchini ikiwemo kupanda Mlima Kilimanjaro.
Magwiji hao wanakuja nchini kwa mwaliko wa kampuni
ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), chini ya Mkurugenzi wake Mkuu, Farough
Baghozah.
Mreno,
Luis Madeil Figo amethibitisha kuja nchini katika ziara hiyo, huku waratibu
wakifanya mawasiliano na wachezaji wengine ili kuangalia uwezekano wa kuwapata.
Miongoni mwa nyota wanaotarajiwa kutua nchini ni
pamoja na Wabrazil Roberto Carlos na Ronaldo De Lima, Mfaransa Zidedine Zidane,
Muitaliano, Fabio Cannavaro, na wengineo.
Vodacom
Tanzania ni miongoni mwa makampuni yaliyojitokeza kudhamini ziara hiyo. Mengine
ni Fastjet, Tropical, Pembe Flower, Lake Gas, EFM Radio na Ladger Plaza Bahari
Beach.
0 comments:
Post a Comment