Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17,
Serengeti Boys jana imelazimisha suluhu pacha ya bila kufungana dhidi ya Afrika Kusini, (Amajimbo) katika mchezo wa
kwanza wa raundi ya pili kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika za vijana.
Mchezo huo ulipigwa katika dimba la kisasa la Azam
Complex, Chamazi, , Mbande, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, dakika 20 za kwanza, Afrika
kusini walitawala na kulisumbua lango la Serengeti Boys, lakini mchezo huo
ukabadilika na vijana wa Tanzania kuanza kusakata soka la uhakika.
Katika kipindi hicho cha kwanza, Serengeti
walipata nafasi mbili za wazi, lakini washambuliaji wake walishindwa kuzibadili
kuwa magoli.
Na katika kipindi cha pili, Serengeti walionekana
kuwa na bahati kwasababu walitengeneza nafasi nyingine mbili za wazi, lakini
washambuliaji walikosa umakini.
Kilichoonekana kwa vijana wa Tanzania ni kuwa na
uoga, lakini kadiri dakika zilivyozidi kukata walitulia na kuweka akili
mchezoni. Kwa Amajimbos walionekana kuwa imara na bora kiufundi, hivyo mchezo
wa marudiano kule Bondeni utakuwa mgumu kwa Serengeti Boys.
Kwa matokeo hayo, kocha mkuu wa Serengeti Boys,
Hababuu Ali ana kazi ya kujiandaa vizuri kwasababu atahitaji ushindi ili
kuwatoa wenyeji kule Afrika kusini au sare ili ya mabao yoyote, kwa maana ya
kufaidika kwa mabao ya ugenini.
0 comments:
Post a Comment