Imechapishwa Julai 26, 2014, saa 6:05 mchana
KOCHA wa Yanga Marcio Maximo
jana amemkaribisha mshambuliaji wa Coventry City inayoshiriki
ligi daraja la kwanza chini Uingereza Selemani Abdallah Mbarouk, kufanya
mazoezi na timu hiyo na endapo atamvutia aweze kumsajili kwa ajili ya
kukitumikia kikosi chake msimu unaokuja
Mbaruku mwenye asili ya Zanzibar,
ameiambia Goal ameichezea kwa kipindi
cha misimu tisa timu hiyo ya Coventry City,na kupata uzoefu wa kutosha kuweza
kuitumikia Yanga endapo Maximo ataridhishwa na kiwango chake.
“Wakala wangu Salimu ambaye nimekuwa
naye tangu nipo kituo cha kukuza vipaji cha Afri Soccer cha Zanzibar ndiyo
amenileta hapa Yanga ameniambia ni timu nzuri ambayo inaweza kunifikisha kule
ambapo ninapataka”alisema Mbarouk.
Mbarouk aliyewahi kupitia Academy ya
Chalsea ya Uingereza akiwa na miaka saba alisema alisifu mazoezi ya Maximo na
uwezo wa wachezaji wa Yanga na kusema anahitaji kujifua zaidi ili aweze
kuendana na kasi yao.
Chanzo: Goal.com
0 comments:
Post a Comment