Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta (aliye na mpira) akifanya vitu vyake dhidi ya Msumbiji mwishoni mwa wiki iliyopita.
Imechapishwa Julai 24, 2014, saa 1:45 asubuhi
KATIKA maisha ya kawaida tu, kila mtu anapenda
kuheshimika na kuthaminiwa na mtu mwingine. Hakuna anayependa kudharauliwa kwa
namna yoyote ile. Heshima ndio kila kitu.
Mtu anapopewa thamani yake ni jambo jema na la
kufurahisha. Hata katika masuala ya kazi, bosi anapoonesha kujali, kuheshimu na
kuthamini kazi ya mfanyakazi, basi huongeza ufanisi wa kazi na kuwapa motisha
zaidi waajiriwa.
Kwa kuwathamini wafanyakazi wako, ni namna nzuri
ya kujipatia mafanikio kwa kampuni au taasisi yoyote ile. Watu watakuwa na
morali ya kufanya kazi na kujitolea ili kukulipa fadhila.
Wachezaji wa soka ni miongoni mwa watu
wanaoheshimika zaidi duniani. Leo hii nani asiyemthamini Cristiano Ronaldo
nchini kwao Ureno au Lionel Messi nchini
Argentina, Neymar kwa Wabrazil? Hawa ni watu wanaothaminiwa sana kwa kazi yao
ya kucheza kabumbu.
Messi anaposafiri kwa ndege kwenda kwao Argentina
kwa ajili ya kuitumikia timu ya taifa, shirikisho la nchi hiyo linamkatia
tiketi ya daraja la juu kama sehemu ya kuthamini ujio na kazi yake.
Unajua kwenye ndege kuna madaraja ya tiketi. Utapata
‘Economy Class’ na ‘Business Class’. Kwa waliobahatika kupanda ndege wanafahamu
madaraja haya vizuri.
Thomas Ulimwengu (kulia) aliwachachafya mabeki wa Msumbiji
‘Economy Class’ ni kwa watu wa kawaida tu, lakini ‘Business
Class’ ni kwa watu fulani wa heshima, hata bei ya tiketi yake imechangamka
kidogo.
Juzi juzi, wachezaji wa kimataifa wa Tanzania
Mbwana Ally Samatta na Thomas Ulimwengu, wanaokipiga klabu ya TP Mazembe nchini DR Congo pamoja na
Mwinyi Kazimoto Mwitula anayecheza klabu ya Al Markhiya ya Qatar walikuja
nchini kuitumikia Taifa Stars.
Stars ilikuwa inakabiliwa na mchezo muhimu wa
kuwania kufuzu hatua ya makundi kusaka
tiketi ya kushiriki fainali za mataifa ya Afrika, AFCON mwakani nchini Morrocco
ambapo mechi ya kwanza ilimalizika kwa sare ya mabao 2-2 ndani ya uwanja wa
Taifa, julai 20 mwaka huu.
Katika mechi hiyo, Samatta, Mwinyi na Ulimwengu
walianzishwa na kocha Mart Nooij. Sasa wanajiandaa kwa mechi ya marudiano itayopigwa
uwanja wa Taifa wa Zimpeto mjini Maputo kati ya Agosti 2 na 3 mwaka huu.
Sasa stori iliyopo kwasasa ni kwamba wakati
wanandinga hao wa kimataifa wanasafiri kuja Tanzania, shirikisho la soka
Tanzania, TFF chini ya Rais Jamal Emil Malinzi liliwafanyia kitu cha thamani
kubwa ndani ya ndege a.k.a Pipa.
Kiungo wa Taifa Stars, Mwinyi Kazimoto (katikati)
Samata, Ulimwengu na Mwinyi walikatiwa tiketi za `Businness Class` kama
ambavyo wachezaji wote wa ukweli duniani wanasafiri ndani ya ‘Business’. Yaani walisafiri
kama vile Messi, Ronaldo, Neymar, na wachezaji wengine wakubwa.
Hali hii imewafurahisa sana akina Mbwana na kuwapa
motisha kubwa ya kuitumikia Taifa Stars.
Wamejisikia kuthaminiwa sana, kiasi kwamba wamepata
morali ya kufanya kazi nzuri. Hawajawahi kupandishwa ‘Business Class’ na
inavyosemekana ndio utakuwa utaratibu ili wasichoke.
Unajua kwenye business Class unaweza kulala kwa
raha ili kupunguza uchovu wa safari.
Hapa TFF mmefanya jambo zuri la kuwathamini
wanandinga wa kimataifa.
Kila la kheri Taifa Stars kuelekea kwenye mechi ya
marudiano mjini Maputo nchini Msumbuji.
0 comments:
Post a Comment