Imechapishwa Julai 24, 2014, saa 12:15 jioni
MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Romelu Lukaku anajifua na klabu yake ya zamani ya Anderlecht kwa lengo la kujiweka fiti kabla ya kuanza msimu mpya wa ligi kuu soka nchini England.
Lukaku bado hajaungana na wachezaji wenzake kutokana na likizo aliyoipata baada ya kutoka katika fainali za kombe la dunia na timu yake ya Taifa ya Ubelgiji.
Karudi nyumbani: Romelu Lukaku ameamua kufanya mazoezi na timu yake ya zamani kabla ya kuanza msimu mpya.
Anatumaini kung`ara: Lukaku atazama zaidi kupata namba ya kudumu katika klabu yake ya Chelsea
Mkali wa mabao: Mshambuliaji wa Ubelgiji, Lukaku alikuwa katika kiwango cha juu na klabu yake ya Everton alipokuwa anacheza kwa mkopo msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment