Imechapishwa Julai 26, 2014, saa 6:25 mchana
MLINDA
mlango wa Liverpool, Pepe Reina amejitia kitanzi mwenyewe katika klabu hiyo,
licha ya kudai anapenda kustaafu soka la kimataifa nchini Hispania.
Akicheza
kwa mkopo Seria A katika klabu ya Napoli msimu uliopita-Reina alianza
kuhusishwa kujiunga na bosi wake wa
zamani wa Anfield Rafael Benitez-na kuzua maswali juu ya hatima yake Liverpool.
Reina
amesisitiza kuwa anaheshimu mkataba wake Anfield-ambao utamalizka mwaka 2016
kabla ya kwenda nchini Hispania.
“Nina
mkataba ambao nahitaji kuuheshimu Liverpool,” Reina aliiambia radio ya Hispania
ya Cadena Ser. “Ninafanya mazoezi vizuri na nipo sawa na wachezaji wenzangu”.
“Nipo
hapa kwa ajili ya kukaa”.
“Sijazungumza
na Brendan Rodgers, ni siku nne tu tangu nifike hapa, naangalia kufanya mazoezi
vizuri ili kurudi katika kiwango changu”.
Reina
mwenye miaka 31 alianza maisha yake ya soka katika klabu ya Barcelona, kabla ya
kwenda Villarreal na kuelekea ligi kuu nchini England, na sasa amekiri kuwa
kurudi La Liga itakuwa nafasi nzuri kwake.
“Nimekuwa
nikiwaza hili kwa muda mrefu kuwa ni vizuri kurudi ulipotoka,” Reina aliongeza.
“Wakati
Rafa Benitez ananisajili Liverpool mwaka 2005, nilikubali na nilisema nitarudi
Hispania baadaye”.
0 comments:
Post a Comment