Kocha Roberto Martinez wa Everton amekamilisha
usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji, Romelu Lukaku aliyeichezea
klabu hiyo kwa mkopo msimu uliopita.
Dili hilo limeigharimu klabu hiyo ya Goodison Park
paundi milioni 28.
Lukaku alijiunga na Chelsea misimu mitatu
iliyopita lakini ameichezea mechi 10 za ligi kuu kabla ya kutolewa kwa mkopo
West Brom na baadaye Everton alikohamia jumla.
0 comments:
Post a Comment