Karibu New York mkongwe: Lampard ametambulishwa rasmi leo na klabu ya New York City.
Imechapishwa Julai 24, 2014, saa 2:21 usiku
MAISHA ya Frank James Lampard katika klabu ya
Chelsea rasmi yamefika tamati baada ya kukamilisha uhamisho wake kujiunga na
New York City inayoshiriki ligi kuu soka nchini Marekani, maarufu kama MLS.
Lampard ametambuliswa rasmi leo klabuni hapo.
Kiungo huyo mwenye miaka 36 ameichezea Chelsea kwa
misimu 13 na kuweka rekodi nzuri ya kuwa mfungaji bora wa kihistoria wa klabu ikiwa ametia kambani mabao 211
Kiungo huyo anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na New
York City FC majira haya ya kiangazi na wa pili mwenye jina kubwa katika
ulimwengu wa soka, baada ya awali kumnasa mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania
David.
Maisha mapya: Frank Lampard alipigwa picha katika uwanja wa ndege wa JFK wakati akiwasili kutambulishwa na New York City FC
0 comments:
Post a Comment