Imechapishwa Julai 23, 2014, saa 5:06 asubuhi
REAL Madrid wametangaza rasmi kumsajili mfungaji bora wa kombe la dunia, James Rodriguez kwa dau la paundi milioni 60 kutoka klabu ya Monaco baada ya kufuzu vipimo vya afya.
REAL Madrid wametangaza rasmi kumsajili mfungaji bora wa kombe la dunia, James Rodriguez kwa dau la paundi milioni 60 kutoka klabu ya Monaco baada ya kufuzu vipimo vya afya.
Nyoya huyo wa kimataifa wa Colombia amekubali kusaini mkataba wa miaka 6 na Real Madrid baada ya kuchukuliwa vipimo vya afya jana asubuhi kabla ya kutangazwa mbele ya mashabiki ndani ya dimba la Santiago Bernabeu.
Rais wa Madrid, Florentino Perez alimkaribisha mshambuliaji huyo na kumfananisha na gwiji wa klabu ,Alfredo Di Stefano aliyejiunga na Real kutokea Colombia.
Amesaini: James Rodriguez alitangazwa jana jioni kuwa mchezaji rasmi wa Real Madrid ndani ya uwanja wa Santiago Bernabeu
Mikono juu: Rodriguez akiwakubali mashabiki waliofurika dimba la Bernabeu wakati akitangazwa kama mchezaji wa Real
Ametua: Rodriguez akipozi katika picha wakati akitambulishwa Santiago Bernabeu
Tabasamu: Rais wa Real Madrid , Florentino Perez (kushoto), Rodriguez (kulia) na mke wake Daniela wakati wa utambulisho.
Muda wa maufundi ukawadia ambapo Rodriguez alionesha uwezo wa juu.
Rodriguez aliwavutia mashabiki Bernabeu
Mambo ya Rodriguez, mfungaiji bora wa kombe la dunia.
Mpenzi? Rodriguez akibusu nembo ya klabu kwenye jezi ya ya Real Madrid
Rodriguez atavaa jezi namba 10 msimu ujao
0 comments:
Post a Comment