Kocha wa Tanzania Prisons, David Mwamwaja akiwa kazini
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Julai 19, 2014, saa 2:40 usiku
MAAFANDE wa jeshi la Magereza, Tanzania Prisons,
maarufu kwa jina la `Wajelajela` wameamua kupunguza kasi ya mazoezi baada ya
shirikisho la soka Tanzania, TFF, kusogeza mbele ligi kuu soka Tanzania bara
mpaka septemba 20 mwaka huu.
Kocha mkuu wa klabu hiyo, Mkongwe, David Mwamwaja
amesema walianza mazoezi mwezi wa sita na walikuwa wanachambua wachezaji ili
wajiunge na timu yao.
“Zoezi la kuchambua wachezaji lilienda vizuri na
likaisha, lakini sasa limekuja suala la kuahirisha ligi, tumeona tupunguze
mazoezi kwasababu hamu ya mpira kwa wachezaji itapungua”
“Nafikiri tutapata nafasi ya kumpuzika ili kupata
nguvu mpya,” . Alisema Mwamwaja.
Kocha huyo alisema amefanya usajili wa wachezaji
wawili tu kwasababu anao vijana wengi aliowapandisha kutoka kikosi cha vijana
chini ya miaka 20.
“Nimemsajili mshambuliaji Amir na mlinda mlango, Mohamed
kutoka JKT Oljoro. Hawa wananitosha na nimezingatia uhitaji wangu”. Alisema
Mwamwaja.
Kwanini ameamua kusajili wachezaji wawili na
kuwapandisha vijana, Mwamwaja alisema kwamba ligi kuu inatisha kwa jina tu,
lakini ni mpira wa kawaida, wachezaji ni wale wale, hivyo ameamua kuchukua
wachezaji kwa nafasi anazohitaji.
Kocha huyo alisema msimu ujao anatarajia kupata
nafasi za juu zikiwemo nafasi ya ubingwa, nafasi ya pili au tatu.
Msimu uliopita, Prisons walinusurika kushuka
daraja na walifanikiwa katika mchezo wa mwisho dhidi ya Ashanti United.
Walimaliza katika nafasi ya 10 kwa kujikusanyia
pointi 28 kibindoni, hivyo kuwaachia majanga ya kushuka daraja, wauza mitumba
wa Ilala, Ashanti United, Maafande wa JKT Oljoro na Rhino Rangers.
Nafasi za timu hizo tatu zilizoshuka daraja zimechukuliwa
na Polisi Morogorogo ya Morogoro, Stand United ya Shinyanga na Ndanda fc ya
mkoani Mtwara.
0 comments:
Post a Comment