Imechapishwa Julai 28, 2014, saa 10:53 jioni
KATIKA historia yake, klabu ya Simba haijawahi kuwa na uwanja
wake wa mazoezi, hivyo kujikuta anahangaika miaka nenda rudi.
Lakini kwasasa unaweza kusema imedhamiria kujenga uwanja wa
mazoezi maeneo ya Bunju jijini Dar es salaam.
Ismail Aden Rage alipokaribia kumaliza muda wake alianza
mchakato wa kujenga uwanja wa Bunju akisema wanataka kupata sehemu ya kufanyia
mazoezi.
Pia alisema wanakusudia kujenga hosteli za kuishi wachezaji
ikiwa ni mkakati wa kupunguza gharama ya kuweka wachezaji hotelini.
Uongozi mpya chini ya Rais Evans Elieza Aveva alisema uko tayari
kuendeleza ujenzi huo ulioanzishwa na Rage.
Mpaka sasa nyasi zilishapandwa na muonekano wa uwanja uko kama
unavyoonekana pichani juu.
0 comments:
Post a Comment