Imechapisha Julai 18, 2014, saa 1:00 asubuhi
NAHODHA wa zamani wa Manchester United na
England, Rio Ferdinand amesaini mkataba wa mwaka mmoja katika klabu ya QPR,
klabu hiyo mpya iliyopanda daraja imethibitisha.
Mtandao wa Goal.com
uliripoti mwezi juni mwaka huu kuwa klabu hiyo iliyopanda ligi kuu ilikuwa na
nia ya kumsaini Ferdinand baada ya kumaliza mkataba na klabu yake ya Man
United.
Ferdinand alithibitisha kuondoka Old Trafford mwezi
mei mwaka huu baada ya kuitumikia timu hiyo kwa miaka 12 ambapo alicheza mechi
454 na alishinda makombe sita ya ligi kuu na ligi ya mabingwa (UEFA) mwaka 2008.
“QPR ni klabu ya kwanza inayocheza ligi kunisajili mimi. Ni kumbukumbu kubwa kwangu-na
kwa familia yangu,” aliuambia mtandao wa klabu hiyo.
“Nilizungumza kwa kirefu na Harry na (mwenyekiti)
Mr (Tony) Fernandes. Nadhani wote walionekana kunikubali na wakaona bado kuna
kitu naweza kufanya-hiyo ndio ilinifanya niwe na hamu ya kuja hapa na kucheza
mpira”.
“Nilikuwa na ofa nyingi duniani kote-baadhi ya sehemu zilikuwa nzuri kuliko
hapa. Lakini malengo yangu yalikuwa kucheza ligi kuu ya England na kurudi hapa
ambapo ilianzia”.
Harry Redknapp alifanya kazi na Ferdinand
wakati beki huyo alikuwa kijana mdogo katika klabu ya West Ham na kocha huyo wa
QPR imefurahi kuungana tena na mkongwe huyo.
“Nimefurahi sana,” aliongeza. “Rio ni mchezaji
mkubwa na waajabu.
Nimefurahi kwasababu tumeweza kumleta hapa”.
“Nilimsajili Rio akiwa na miaka 14. Muda wote akiwa
ndani na nje ya uwanja alipenda kujifunza, ameendelea kufanya hivyo katika
maisha yake yote ya mpira”.
“Wakati anacheza Manchester United, alikuwa ndiye beki bora barani Ulaya, kama sio
dunia nzima”.
0 comments:
Post a Comment