Imechapishwa Julai 21, 2014, saa 10:03 jioni
LIVERPOOL imethibitisha kumtoa kwa mkopo, Iago Aspas katika klabu ya Sevilla ili aicheze
kwa msimu wa 2014/2015.
Mshambuliaji huyo alijiunga na wekundu wa Anfield
kutoka CeltaVigo majira ya kiangazi mwaka jana, lakini ameshindwa kuingia timu
ya kwanza na amecheza mechi 15 katika mashindano yote.
Sevilla alitangaza kukamilika kwa dili hilo wiki
iliyopita na kusema kuwa watafanya mpango wa kumsajili kwa mkataba wa kudumu mchezaji
huyo mwenye miaka 26.
Nafasi yake katika klabu imedhoofishwa zaidi na
Brendan Rodgers baada ya kumsajili Adam Lallana, Rickie Lambert na Lazar
Markovic, japokuwa Luis Suarez ameuzwa.
Aspas aliifungia Liverpool goli pekee katika
mchezo wa raundi ya tatu ya kombe la FA mwezi januari.
Lucas Leiva naye anatarajia kuondoka Anfield kwa
mkopo na kujiunga na Napoli ambayo inakaribia kumsajili kiungo huyo wa Brazil.
Pia Liverpool wamekubali kumuuza Fabio Borini
katika klabu ya Sunderland na kichobaki ni makubaliano binafsi na mchezaji.
0 comments:
Post a Comment