Athuman Idd 'Chuji' baada ya kuikosa Azam fc sasa anasaka nafasi ya kusajiliwa JKT Ruvu
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Julai 30, 2014, saa 10:48 jioni
WANANDINGA waliotamba na klabu za Yanga, Simba na
Azam fc wanafanya majaribio chini ya kocha mkuu wa JKT Ruvu, Fredy Felix
Minziro kwa lengo la kutafuta nafasi ya kusajiliwa kwa ajili ya msimu wa
2014/2015 wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Meneja wa JKT Ruvu, Joel Frank Cibaya ameiambia
MPENJA BLOG jioni hii kuwa wachezaji wanaofanya mazoezi kwa muda mrefu sasa ni Henry
Joseph Shindika, Haruna Ramadhani Shamte, Betram Mombeki na Jackson Chove.
Pia Cibaya alimtaja aliyekuwa kiungo mahiri wa
Yanga, Athuman Idd `Chuji` kuwa anajitokeza mara kadhaa katika mazoezi hayo.
Betram Mombeki kutoka Simba sc anaendelea kujaribu bahati yake JKT Ruvu.
“Wapo wachezaji wanaofanya mazoezi hapa. Na kwa
bahati nzuri TFF wamesogeza ligi mbele imekuwa ni nafasi nzuri ya kuwaangalia,”Alisema
Cibaya.
“Mwalimu kuna wachezaji anawatazamia. Kama
unavyojua ana uzoefu na wachezaji wa timu kubwa. Hakuna watu wasumbufu kama
wachezaji wa timu kubwa hususani kutoka Simba na Yanga”
“ Kwasababu wale hawaamini kama wapo JKT Ruvu au
wako Mtibwa. Wanadhani maisha ya Simba na Yanga ndio yapo JKT Ruvu, kwahiyo
wanapovikosa vitu walivyopata Simba wanakuwa wasumbufu zaidi”.
Katika hatua nyingine, Cibaya aliwataja wachezaji
waliosajiliwa kwa maana ya raia na askari kuelekea msimu mpya wa ligi kuu
unaotarajia kuanza kutimua vumbi septemba 30 mwaka huu.
Jabir Aziz (kushoto) anafanya majaribio JKT Ruvu
Wachezaji raia waliosajiliwa na JKT Ruvu ni:
Ambrose Morris (kutoka Zanzibar), Mohamed Faki (Ashanti) na Benjamin Haule
(Ruvu Shooting).
Wachezaji askari (wanajeshi) waliosajiliwa ni:
Madenge Ramadhani, Issa Kanduru, Nafo Sanane na Nurdin Mohamed (wote kutoka JKT
Oljoro).
Cibaya aliwataja wachezaji wawili waliostaafu soka
kuwa ni Hussein Bunu na Sostenesi Manyasi.
Aidha, aliwataja wachezaji askari walioachwa na
kupelekwa JKT Oljoro kwa mkopo kuwa ni: Abdallah Bunu, Stanley Mkomola, Bakari
Kondo, kessy Mapande Paulo Ndamko.
Cibaya aliongeza kuwa wapo wachezaji raia
walioachwa na klabu hiyo ambao ni: Omary Kapilima, Kalage Mgunda, Jamal
Machelanga, Emmanuel Swita, Sadick Mecky, Omary Mtaka, Stanley Mkomola, Salum Machaku
na Chacha Marwa.
Kuhusu maandalizi ya msimu ujao, Cibaya alisema
wanaendelea vizuri kupanga majeshi yao ili kufanya vyema tofauti na msimu
uliopita.
“Sisi tunaendelea vizuri na maandalizi, kama
unakumbuka hapa katikati tulikuwa na majaribio na kufanikisha kupata wachezaji
mbalimbali,”
“Kwasasa tunaandaa timu ya wakubwa na wadogo.
Tumefanya hivyo kama miezi mitatu au miwili na nusu. Tumepata wachezaji wadogo
wazuri, kama ulikuwa unafuatilia tumefika mpaka robo fainali ya mashindano ya
Rolling Stone”. Alisema Cibaya.
0 comments:
Post a Comment