Marafiki: Nemanja Vidic akimiliki mpira mbele ya mshambuliaji wa Manchester United, Danny Welbeck.
Imechapishwa Julai 30, 2014, saa 4:56 asubuhi
Nemanja Vidic amefichua siri kuwa alipata ofa nyingi baada ya kutangaza maamuzi ya kuondoka Manchester United, ikiwemo klabu za England.
Mserbia huyo alitangaza maamuzi ya kuondoka Old Trafford mwezi februari mwaka huu baaada ya kucheza kwa miaka 8.
Vidic alikubali kujiunga na Inter Milan mwezi machi mwaka huu kufuatia mkataba wake kumalizika majira ya kiangazi mwaka huu.
Katika mohajiano yaliyojaa hisia na MUTV kueleka mchezo wa jana baina ya Man United na Inter mjini Washington D.C., ambapo United walishinda kwa penalti 5-3, beki huyo alisema: 'Nilikuwa na ofa nyingi kutoka mataifa tofauti, hata kutoka England. Inter ipo wakati wa mpito, inajitahidi kujiimarisha, lakini nimependa mpango wao. Inter itakuwa kubwa na kubwa zaidi , naamini nitawasaidia kufikia malengo yao".
Vidic akimuonesha ufundi mchezaji mwenzake wa zamani wa Man United, Danny Welbeck.
Vidic ambaye mara nyingi anapenda kutumia neno 'sisi' kila anapoizungumzia United, pia anaamini klabu yake ya zamani itaimarika zaidi chini ya kocha Louis Van Gaal baada ya kutimuliwa kazi kwa David Moyes.
"Ikiiangalia klabu kwa sasa, ipo wakati wa mpito. Wachezaji wapya wanaingia, Sisi (United) tumebadili makocha, wa kwanza David Moyes na sasa Louis Van Gaal na hata mkurugenzi alibadilishwa baada ya mwaka jana David Gill kuondoka na ( Ed Woodward alipandishwa)'
'Natumaini mwaka huu ni muhimu kwao na wachezaji waliosubiri nafasi watapata nafasi ya kuingia kikosini. Wachezaji wapo tayari kwa nafasi".
0 comments:
Post a Comment