Thursday, July 31, 2014

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

Imechapishwa Julai 31, 2014, saa 2:46 asubuhi

NDANDA fc ya Mtwara inaingia kambini leo kuendelea kujiwinda na mikikimikiki ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015 inayotarajia kuanza kushika kasi septemba 20 mwaka huu.

Katibu mkuu wa klabu hiyo, Seleman Kuchele ameimbia MPENJA BLOG kuwa kwa kiasi kikubwa wamekamilisha ripoti ya kocha wao aliyokabidhi baada ya kumalizika kwa ligi daraja la kwanza, na wamebakiza nafasi mbili tu za usajili.

“Sisi tunaendelea kuikamilisha ripoti ya mwalimu. Kocha alikuwa anahitaji wachezaji tisa na mpaka sasa hivi tumesajili wachezaji saba na wawili tupo katika mipango ya mwisho na kwasababu muda umeongezwa, tutakuwa katika wakati mzuri wa kukamilisha,” Alisema Kuchele.

“Hawa wachezaji wawili tumewapata, wanatoka timu za ligi kuu,

‘. Alisema Kuchele. “ Mazungumzo yamekamilika na kilichobaki ni kumalizana nao,”

Kuchele aliongeza kuwa katika ripoti ya kocha, alihitaji wiki nane za mazoezi na uongozi umelifanyia kazi hilo kwasababu walianza mazoezi ya kwanza, lakini wakatoa likizo ya wiki moja kwa ajili ya sikukuu ya Eid na leo wanaanza kambi rasmi ya maandalizi.

Kuchele aliwataja wachezaji waliowasajili kuwa ni Paul Ngalema kutoka (Mtibwa Sugar), Ernest Joseph (Kagera Sugar), Jacob Masawe (JKT Oljoro), Khamis Saleh (JKT Oljoro), John Brown  (Rhino Rangers),  Boniface Mwenda (Prison) na Omary Nyenje (kutokea kikosi cha maboresho ya Taifa stars).

Katibu huyo alisisitiza kuwa Ndanda fc ni timu ya wananchi, hivyo wanajiandaa kwa nguvu zote ili kutowaangusha mashabiki wake.

“Kwanza tuna deni kubwa na watu wa Mtwara, kwasababu mapokezi waliyotupa ni makubwa, tunalo deni la kuhakikisha hatuwaangushi kwa kuleta ushindani ligi kuu,” Aliongeza Kuchele. “Kwa wakati huu tuna mpango wa kushika nafasi tatu za juu, lakini baada ya miaka mitatu tunahitaji kuchukua ubingwa kwa mujibu wa programu ya timu,”


“Tunawaomba watu michango yao ya hali na mali ili tuweze kufikia malengo yetu,”

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video