Amegusa ardhi: Luis Suarez alipigwa picha akiwasili Barcelona jumatatu usiku .
Imechapishwa Julai 15, 2014, saa 12:19 jioni
LUIS Suarez alipigwa picha jana jumatatu akiwasil Barcelona pamoja na mke wake na mtoto wao wa kike baada ya kukamilisha uhamisho wa paundi milioni 75 akitokea Liverpool.
Mshambuliaji huyo wa Uruguay alikanyaga ardhi ya Katalunya mapema asubuhi na atakamilisha kila kitu katika uhamisho wake.
Suarez ameondoka Liverpool na kujiunga na La Liga. Ikumbukwe nyota huyo mtukutu alijiunga na majooo wa jiji mwezi januari mwaka 2011 akitokea klabu ya Ajax.
FIFA walithibitisha kuwa Barcelona hawaruhusiwi kumtangaza rasmi hadharani kutokana na kifungo cha miezi minne.
Siku za nyuma, Wakatalunya walitangaza usajili wa Neymar na Fabregas katika dimba lao la Camp Nou lililofurika mashabiki.
Muuruguay huyo atakamilisha usajili wake wa paundi milioni 75 kujiunga na Barcelona.
Safari: Suarez hatakiwi kutangazwa hadharani wakati huu anaitumikia adhabu ya kufungiwa miezi minne.
Dole: Suarez akiwa katika jezi maarufu ya Katalunya.
Kulikuwa na taarifa kuwa Barcelona walitaka kumtangaza hadharani Suarez kwenye uwanja usiokuwa wa michezo wakati huu amefungiwa miezi minne, lakini FIFA walithibitisha kuwa tukio kama hilo halitaruhusiwa wakati adhabu inaendelea.
Msemaji wa FIFA Delia Fischer alisema: "Kifungo kinahusu shughuli zote zinazohusiana na mpira. Hawezi kuwa katika tukio linalohusiana na mpira. Hawezi hata kushiriki shughuli za kijamii zinazohusiana na mpira".
0 comments:
Post a Comment