Imechapishwa Julai 20, 2014, saa 7:43 mchana
LOUIS van Gaal na wachezaji wake wa Manchester United wapo katika morali kubwa kwenye ziara yao nchini Marekani.
Mholanzi huyo alionekana kucheka na kutaniana na mshambuliaji wake, Wayne Mark Rooney, wakati wachezaji wapya Luke Shaw na Ander Herera wakipata nafasi ya kuwajua wachezaji wenzao.
Man United wamepigga kambi ya maandalizi ya msimu mpya huko Marekani na sasa wanajiandaa na mechi ya kirafiki jumatano ijayo dhidi ya LA Galaxy.
Van Gaal na Rooney walionaka kuelewana vizuri ambao mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England alikuwa anamtania bosi wake mpya.
Hapa kazi tu mzee wangu!: Van Gaal akitabasamu wakati akimtazama Rooney ambaye pia alifurahi.
Mwanzo mzuri: Kambi ya Man United ilionekana kuwa na furaha jumamosi mjini Los Angeles
Anasaka pumzi: mchezaji aliyesajiliwa kwa paundi milioni 30, Luke Shaw, kushoto, akifanya mazoezi na wenzake
Ander Herrera, kulia, alipata nafasi ya kuonesha ufiti wake kwa kocha wake na wachezaji wenzake
Herrera na Mata wakinyosha viungo
Kinda: Reece James ni miongoni mwa wachezaji wa Akademi walioitwa katika ziara ya Marekani.
0 comments:
Post a Comment