Saturday, July 19, 2014

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam


WEKUNDU wa Msimbazi Simba wanatarajia kukipiga na Ismailia ya Misri au Zesco ya Zambia katika tamasha la klabu hiyo maarufu kama `Simba Day`, Agosti 9 mwaka huu ndani ya dimba la Taifa jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange `Kaburu` katika mkutano wake na waandishi wa habari leo makao makuu ya klabu hiyo, mtaa wa Msimbazi, Kariakoo, jijini Dar es salaam, amesema  nia yao ni Ismailia na kama mipango haitaenda sawa basi wataialika Zesco ya Zambia.

Tamasha la Simba ni maarufu nchini na linawapa nafasi mashabiki wa klabu hiyo kuwaona wachezaji wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu mpya.

‘Siku ya tarehe 9 tutatambulisha jezi, kikosi chetu cha kwanza na kikosi cha chini ya vijana wa miaka 20”. Alisema Kaburu.

Wachezaji nao inakuwa faida kubwa kwao kwasababu wanapata fursa ya kujitambulisha mbele ya mashabiki wao.

Wakati huo huo, Kaburu alisema usajili unakwenda vizuri na kesho kamati ya usajili inayoongozwa na kepteini za zamani wa jeshi la wananchi wa Tanzania, JTWZ, Zacharia Hans Poppe itakutana kujadili masuala kadhaa.

Kuhusu beki wake raia wa Burundi, Gilbert Kaze, Kaburu alisema wameshapokea barua akiomba kujiunga na klabu yake ya zamani Vital`O.

Awali mwenyekiti wa kamati ya usajili, Hans Poppe aliwahi kuweka wazi na kukaririwa na mtandao huu akisema waliamua kuachana na Kaze baada ya kuona ana majeruhi ya muda mrefu.

Poppe alisema haikuwa rahisi kwa Kaze kurudi uwanjani msimu ujao, hivyo hawakuona haja ya kuendelea kuwa naye. Lakini alisema watafuata taratibu zote na kuongea naye kuhusu hilo.

Leo Kaburu amethibitisha kuwa uongozi umekubali maombi ya Kaze na sasa Mrundi huyo atarudi kwao kwasababu hana nafasi katika kikosi cha Simba.

Kaburu aliongeza kuwa beki wao Hassan Hatibu anatakiwa na Kagera Sugar na wamekubalia maombi hayo kwasababu hana nafasi pia, waati huo huo, alisema wamekubali kuondoka kwa mshambuliaji wao, Betram Mwombeki aliyejiunga na JKT Ruvu ya mkoani Pwani.

Kuhusu wanachama 69 waliosimamishwa uanachama kwa sababu ya kwenda mahakamani, Kaburu alisema wanachama hao wametumiwa barua ya kutakiwa kufika katika mkutano mkuu wa Agosti 3 mwaka huu.


Hata hivyo alisema suala la Wambura aliyesimamishwa uanachama kwa kosa kama hilo mwaka 2010, naye suala lake litapelekwa katika mkutano huo na wanachama wataamua hatima kwa mujibu wa katiba. Pia amesema wanachama watakapopata taarifa rasmi, wasikose katika mkutano huo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video