Ana furaha katika rangi nyekundu na nyeusi: Mario Balotelli anaonekana kama vile ataondoka katika klabu ya AC Milan majira haya ya kiangazi.
Imechapishwa Julai 26, 2014, saa 7:45 mchana
DHAMIRA ya Arsenal kutaka kumsajili Mario Balotelli inaonekana kufa , baada ya Mkurugenzi wa AC Milan, Adriano Galliani kudai mshambuliaji huyo mtukutu atabakia klabuni hapo.
Mshambuliaji huyo wa kati wa zamani wa Manchester City amekuwa akihusishwa kujiunga na Aserne Wenger na hata Rais wa Ac Milan, Silvio Berlusconi alikaririwa mapema majira ya kiangazi akisema: 'Nilikuwa namuuza Balotelli kwa timu za England kwa mamilioni ya fedha".
Hata hivyo, Galliani amejitokeza na kusema hakuna uwezekano wa nyota huyo kutua England kwasababu mshambuliaji huyo mwenye miaka 23 yupo katika mipango ya klabu msimu ujao.
Mshindi: Balotelli akishangilia baada ya kufunga bao la ushindi katika mchezo wa kombe la dunia hatua ya makundi dhidi ya England.
'Balotelli kamwe hajawahi kuomba kuuzwa,' Alisema Galliani. 'Kuna asilimia 99.9% ana nafasi ya kubakia hapa, lakini huwezi kujua nini kitatokea".
Japokuwa washika bundiki hawajapoteza nafasi kwasababu Mkurugenzi wa Milan aliwahi kusema hivyo hivyo kuhusiana na Mbrazil Kaka, akisema: 'Ni kweli tutambakisha hapa. Nina asilimia 99.9%, atabakia hapa'.
Lakini Kaka aliondoka na kujiunga na Orlando City kwa mkopo kupitia klabu ya Sao Paulo.
Lakini Wenger alikaririwa akisema anafurahia wachezaji alionao safu ya ushambuliaji na kuonekana kama vile amepiga chini dili la kumsajili Balotelli majira haya ya kiangazi mwaka huu.
Yeye tena: Nyota wa zamani wa Man City, Mario Balotelli (kushoto) amekuwa akihusishwa kujiunga na Asernal.
0 comments:
Post a Comment