Imechapishwa Julai 22, 2014, saa 4:00 asubuhi
WAKATI mabishano ya kama kweli Lionel Messi
alistahili tuzo ya mchezaji bora wa kombe la dunia 2014 nchini Brazil yakipoa
`mdogo mdogo`, mchezaji mwenzake wa Barcelona, Sergi Roberto ameibuka tena
akisema jamaa yake alistahili kutwaa tuzo hiyo.
Nyota huyo wa Argentina aliyaanza kwa kasi
mashindano yaliyomalizika Brazil, lakini alizimika kadiri mashindano
yalivyoendelea na alikuwa mchezaji tegemeo katika kipigo cha bao 1-0 dhidi ya
Ujerumani, mechi ya fainali uwanja wa Maracana.
Licha ya nyota huyo mwenye miaka 27 kutajwa kuwa
mchezaji bora wa kombe la dunia-maamuzi ya kumpa tuzo hiyo yalipokolewa kwa hisia
tofauti na wachezaji, makocha na mashabiki wa soka duniani kote.
Ingawa kwa upande wa Roberto bado ana msimamo kuwa
Messi alistahili tuzo hiyo na ametaka aheshimiwe kwa kiwango chake.
“Nilimuona Messi kombe la dunia kama ilivyokuwa
miaka mitatu iliyopita,lakini mwaka huu alikuwa kwenye ubora wake.” Aliwaambia
waandishi wa habari.
“Anastahili zawadi na kumkosoa sio haki, alitaka
kushinda kombe la dunia, anastahili heshima kubwa. Ameisaidia sana klabu yake
na Argentina”.
Roberto mwenye miaka 22, pia aliwasifu Real Madrid
kwa usajili wa karibuni wa Toni Kroos kwa kuzingatia ubora wake wa siku za
karibuni katika kikosi cha Bayern na timu ya Taifa ya Ujerumani.
“Ni mchezaji mzuri sana, amethibitisha hilo kombe
la dunia na klabu ya Bayern. Hajajiunga na sisi, lakini mchezaji yeyote bora
anakaribishwa Barcelona”.
0 comments:
Post a Comment