Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Julai 31, 2014, saa 1:53 usiku
KOCHA mkuu wa Yanga sc, Mbrazil,
Marcio Maximo kesho anaweza kuwataja wachezaji atakaowatumia katika michuano ya
kombe la Kagame itakayofanyika mjini Kigali, Rwanda kuanzia Agosti 8 mwaka huu.
Katibu mkuu wa Yanga, Beno Njovu
amesema Maximo atazungumza na waandishi wa habari kesho baada ya mazoezi katika
uwanja wa shule ya sekondari ya Loyola, Mabibo jijini Dar es salaam, hivyo anaweza
kudokeza wachezaji atakoenda nao Rwanda.
“Kesho mwalimu ataongea na waandishi wa habari, kwahiyo yawezekana
akatoa dalili ya wachezaji gani anaweza kuwatumia kombe la Kagame,” alisema Njovu.
“Hasa ukizingatia mwishoni mwa wiki
timu nyingi za taifa zitakuwa na mechi, kwahiyo yawezekana wachezaji wengi
wakawa hawajawasili, mpaka terehe ya safari yetu, hivyo mwalimu akashindwa
kuwatumia.
Njovu alisema kwa vile michuano
inaanza Agosti 8, wanajipanga kuondoka nchini Agosti 5, ingawa bado hawana
uhakika.
Kuhusu mchezaji wa kigeni atayeachwa
kati ya Emmanuel Okwi, Khamis Kiiza na Haruna Niyonzima baada ya kusajiliwa kwa
Wabrazil wawili, Andrey Coutinho na Gleison Santos Santana ‘Jaja’, Njovu alisema mpaka sasa mwalimu hajafikia
mamuzi ya nani anapunguzwa.
“Mwalimu atathibitisha baada ya
kuwaona wachezaji hawa wote wakifanya mazoezi pamoja na kuona ni kombinesheni
ipi itamfaa, hapo ndipo ataamua ni mchezaji gani anaachwa, hata kama
itasikitisha”
“Bado muda tunao, mwalimu anaweza
kumtema mchezaji hata baada ya kombe la Kagame kwa maana ya kwamba atakuwa
amepata muda mzuri wa kuwaona wachezaji hao”. Aliongeza Njovu.
0 comments:
Post a Comment