Baada ya
Maximo kumsajili Jaja Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo wamekuwa wakiumiza
kichwa kutaka kujua mchezaji gani kati ya Kiiza na Okwi atakatwa kwenye usajili
Imechapishwa Julai 26, 2014, saa 6:31 mchana
KOCHA wa Yanga Marcio Maximo amesema pamoja na kumpa
mkataba wa miaka miwili Mshambuliaji Geilson Santana Santos ‘Jaja’lakini bado
anahitaji kuona uwezo wa washambuliaji wawili raia wa Uganda Hamisi Kiiza na
Emmanueli Okwi.
Maximo ameiambia Goal kwamba anataka kuwa na timu imara
itakayohitaji wa wachezaji wote na siyo mchezaji mmoja mmoja kama zilivyo
baadhi ya timu nyingine ambazo ikitokea mchezaji huyo anaumwa zinashindwa
kufanya vizuri.
“Nalazimika kuwaona mazoezini Okwi na Kiiza ndiyo nitakuwa
na jibu la kusema lakini kwa sasa bado ni mapema mno kusema nitampunguza nani
kwa sababu hata katika rekodi za klabu naona wachezaji hawa wamekuwa na mchango
mkubwa ndani ya timu ukitoa usumbufu ambao inasemekana wanao,”alisema Maximo.
Baada ya Maximo kumsajili Jaja Wanachama na Mashabiki wa
timu hiyo wamekuwa wakiumiza kichwa kutaka kujua mchezaji gani kati ya Kiiza na
Okwi atakatwa kwenye usajili wa msimu ujao huku kila mtu akiwa na mapendekezo
yake.
Chanzo:Goal.com
0 comments:
Post a Comment