Hajavutiwa: Manuel Pellegrini ameipiga chini ofa ya kurithi mikoba ya Luiz Felipe Scolari .
Imechapishwa Julai 16, 2014, saa 11:25 alfajiri
KOCHA wa Manchester City, Manuel Pellegrini amekataa ofa ya kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Brazil, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Chile.
Inaelezwa kuwa Pellegrini alifuatwa wakati wa mechi ya fainali ya kombe la dunia siku ya jumapili, saa 24 kabla ya Luiz Felipe Scolari kuachishwa kazi kutokana na matokeo mabaya ya Brazil katika mashindano hayo yaliyofanyika katika ardhi yake.
Brazil ilifungwa mabao 7-1 katika mchezo wa nusu fainali na Ujerumani na ikafungwa mabao 3-0 dhidi ya Uholanzi kwenye mechi ya kutafuta mshindi wa tatu.
Ingawa inasemekana kuwa Pellegrini amegoma kuingia katika makubaliano na shirikisho la soka nchini Brazil, amesisitiza kuwa anahitaji kuona miaka yake yake mitatu iliyosalia katika mkataba wake ndani ya dimba la Etihad.
Mafanikio: Pellegrini alishinda kombe la ligi kuu na kombe la Capital One Cup katika msimu wake wa kwanza ndani ya klabu ya City.
Pellegrini na kikosi chake wapo katika mazoezi ya wiki moja, St Andrews nchini Scotland kabla ya kucheza mechi yao ya pili ya kujipima ubavu dhidi ya Hearts siku ya ijumaa.
Naye mkurugenzi wa michezo, Txiki Begiristain inasemekana anatakiwa, japokuwa haijawekwa wazi kama tayari ameshafuatwa na Brazil kwa mazungumzo.
Kimeota nyasi: Scolari hajaongezewa mkataba mwingine baada ya Brazil kumaliza nafasi ya nne katika fainali za kombe la dunia za mwaka 2014.
Wazee wa kipigo: Scolari aliambulia vipigo vya aibu kutoka kwa Ujerumani na Uholanzi.
Mtu maarufu: Pellegrini anapendwa na wachezaji nyota katika kikosi cha Man City.
0 comments:
Post a Comment