Dedryck Boyata akiruka juu na kupiga kichwa kuipa Man City bao lililofanya ubao wa magoli kusomeka 2-1 kabla ya mapumziko.
Mwanzo mzuri: Mchezaji mpya wa Man City, Bruno Zuculini akifunga bao la kuongoza dhidi ya Kansas.
Imechapishwa Julai 23, 2014, saa 2:20 asubuhi
SI Bruno Zuculini au Kelechi Iheanacho aliyesajiliwa rasmi kujiunga na mabingwa wa England, Manchester City, lakini wote walifunga mabao kwenye mchezo wa kirafiki nchini Marekani.
Man city waliopo ziarani nchini Marekani waliibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Sporting Kansas City.
Zuculini atajiunga rasmi na City kwa dau la paundi milioni 1.5 kutokea klabu ya Racing Club na mchezaji mwenye thamani kubwa wa Nigeria Iheanacho anaonekana kuwa katika majaribio kwenye ziara hiyo ya Marekani.
Mabao ya Man City yalifungwa na Zuculini dakika ya 3, Boyata dakika ya 45, Kolarov kwa penati dakika 73, na Iheanacho katika dakika ya 89.
Bao la Sporting Kansas City lilifungwa na Sapong katika dakika ya 30.
0 comments:
Post a Comment