Wednesday, July 23, 2014

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam


Imechapishwa Julai 23, 2014, saa 2:19 usiku

AZAM FC inatarajia kucheza mechi ya kujipima uwezo kesho asubuhi dhidi ya maafande wa jeshi la kujenga taifa kutoka mkoani Pwania, Ruvu Shooting katika uwanja wa Azam Complex.

Afisa habari wa klabu hiyo, Jafar Idd Maganga amesema kikosi cha Azam kinaendelea vizuri na mazoezi chini ya kocha mkuu, Mcameroon, Joseph Marius Omog ambapo kila wiki wanahitaji kucheza mechi ya kirafiki.

“Tunaendelea vizuri na mazoezi. Ushindani umekuwa mkubwa kwa wachezaji. Unajua kipindi hiki ni kigumu kwa wachezaji, kila mtu anahitaji kufanya vizuri ili kupata namba”. Alisema Jafar.

“Tumekuwa tukicheza mechi za kirafiki kwa lengo la kujua kama wachezaji wanaelewa yale yanayofundishwa”.

“ Kwahiyo kesho tutakuwa na mechi ya kirafiki dhidi ya Ruvu Shooting, moja ya timu nzuri, yenye vijana wenye uwezo mkubwa. Wao watasafiri kuja kwetu”. Aliongeza Jafar.

Kikosi cha Ruvu Shooting msimu uliopita

“Tumesajili wachezaji wengine, wote wanaonesha kiwango kizuri. Hivyo inaonesha kutakuwa na ushindani mkubwa kikosini”.

Aidha, Jafar aliongeza kuwa kocha mkuu Omog ameamua kuahirisha mpango wa kwendea nje ya nchi kuweka kambi, badala yake kwa muda uliobaki wataendelea kufanya mazoezi Chamazi na kucheza mechi za kirafiki.

Kwa upande wao, Ruvu Shooting walisema maandalizi kwa ajili ya mechi hiyo yamekamilika na kesho watawaonesha mabingwa hao wa ligi kuu namna ya kucheza soka.


Afisa habari wa klabu hiyo, Masau Bwire alisema kikosi chao kipo vizuri baada ya kusajili wachezaji kadhaa, hivyo kesho watawaonesha Azam kuwa wao ni watu makini.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video