Seko Fofana (Jezi namba 8) alimpiga mchezaji wa kNHK Rijeka baada ya kubaguliwa.
Imechapishwa Julai 23, 2014, saa 6:32 mchana
Patrick Vieira alikuwa sahihi kukitoa nje ya uwanja kikosi cha wachezaji wa timu ya vijana ya Manchester City baada ya wanandinga wake kuoneshwa vitendo vya ubaguzi wa rangi, amesema kocha Manuel Pellegrini.
Vieira alisimamisha mechi dhidi ya NHK Rijeka katika ziara yao nchini Croatia kujiandaa na msimu mpya baada ya kinda mwenye miaka 19, Mfaransa, Seko Fofana kubaguliwa.
Pellegrini alisema: 'Sijui sana kuhusu hilo, lakini kama Patrick aliona ni sahihi kuwatoa uwanjani wachezaji, basi itakuwa kitu sahihi'.
Kadi nyekundu: Fofana alioneshwa kadi nyekundu baada ya kumpiga mpinzani wake
Alionesha msimamo: Patrick Vieira (wa tatu kushoto) akiingia uwanjani baada ya kusikia kilichotokea.
Ngoma imeisha: Mechi iliahirishwa baada ya Vieira kuwaongoza wachezaji wake kutoka nje ya uwanja nchini Croatia
'Alitathimini hali halisi na alifanya kitu sahihi. Haiwezekani kuendelea kucheza wakati kitu kama hiki kimetokea'.
Fofana alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga mpinzani wake, lakini klabu imeeleza imani yake kuwa Fofana, kijana mwenye kipaji kikubwa, alibaguliwa kabla ya kutokea kwa tukio hilo. Tukio hilo lilitokea kabla ya mapumziko.
Maamuzi ya kuahirisha mechi yalichukuliwa na viongozi waliokuwa na kikosi hicho na Vieira aliamua kumuunga mkono kinda huyo kwasababu alikuwa na mawazo mengi kutokana na tukio hilo.
Taarifa ya klabu jana jioni ilisomeka: 'Kikosi cha vijana chini ya miaka 20 cha Manchester City kilikuwa na mchezo dhidi ya HNK Rijeka leo (jumanne) na imeahirishwa kutokana na tukio la kiungo kijana, Seko Fofana kubaguliwa na mchezaji wa timu pinzani'.
Kinda: Fofana akiwa akionesha vitu vyake katika mechi dhidi ya Chelsea ya vijana chini ya miaka 21 msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment