Wasiwasi: Presha ya Luiz Felipe Scolari ilikuwa kubwa baada ya kupoteza kwa kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Uholanzi.
Imechapishwa Julai 14, 2014, saa 8:13 mchana
Luiz Felipe Scolari Kibarua chake kimeota nyasi baada ya wenyeji Brazil kufungwa mara mbili mfululizo ndani ya siku tano.
Brazil walishindwa kupata ushindi siku ya jumamosi katika mechi ya mshindi wa tatu ambapo walifungwa mabao 3-0 na Uholanzi, huku tayari walikuwa wanaugulia kipigo cha mabao 7-1 kutoka kwa Ujerumani katika mchezo wa nusu fainali jumanne ya wiki iliyopita.
Japokuwa haijatangazwa rasmi, vyombo vya habari vya Brazil vinaripoti kuwa Scolari amefukuzwa kazi.
Kocha huyo alikutana na viongozi wa shirikisho la soka nchini Brazil jumamosi usiku baada ya kupoteza mechi, na kuwasababisha wapoteze mechi mbili mfululizo katika ardhi yao tangu mwaka 1940.
Majanga mengine: Scolari ameachishwa kazi baada ya Brazil kupoteza mechi dhidi ya Brazil katika mechi ya mshindi wa tatu
Dalili: Shabiki wa Brazil akimshukuru Scolari kwa kuwapa ubingwa mwaka 2002, lakini amemtaka kuondoka.
0 comments:
Post a Comment