Kazi inaendelea: Shinji Kagawa, Darren Fletcher na Tom Cleverley, wafungaji wanne wa penati za United, wakishangilia ushindi wao wa penalti 5-3 dhidi ya Inter Milan.
Imechapishwa Julai 30, 2014, saa 4:10 asubuhi
KOCHA Louis van Gaal ameendelea kufanya vizuri kufuatia Manchester United kuitandika kwa penalti 5-3 Inter Milan baada ya sare ya 0-0 katika mechi ya Kombe la Kimataifa kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani.
Katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa FedEx Field mjini Washington, penati za Man United zilizamishwa kambani na Ashley Young, Javier Hernandez, Tom Cleverley, Shinji Kagawa na Darren Fletcher wakati Marco Andreolli wa Inter aligongesha mwamba.
ziara hiyo ya Marekana imekuwa ya mafanikio kwa Van Gaal kwani ameshinda mechi tatu mfululizo na wachezaji wake wamepata nafasi ya kumuonesha uwezo, hivyo lawama hazitegemewi.
Kocha huyo mpya wa United anaendelea kutafuta njia ya kuutekeleza mfumo wake anaoupenda wa 3-5-2.
Kwa mfano jana usiku, Man United walianza mchezo na washambuliaji wawili, Wayne Rooney na Danny Welbeck. Walimaliza mchezo na Nani na Wilfried Zaha katika nafasi hizo.
Fletcher akishangilia ushindi na kipa wa United David De Gea baada ya kushinda kwa penalti na kumpa Van Gaal rekodi ya ushindi wa asilimia 100 katika michuano hiyo.
Furaha: Louis van Gaal na Ryan Giggs wakitabasamu baada ya ushindi
Fletcher akimkumbatia Michael Keane baada ya kufunga penalti mjini Washington.
Katika mchezo huo, kocha Van Gaal alichezesha vikosi viwili.
Kikosi cha Manchester United kipindi cha kwanza half: Lindegaard, Smalling, Jones, Evans, Valencia, Fletcher, Herrera, Young, Mata, Rooney, Welbeck
Kipindi cha pili: De Gea; M Keane, Evans, Blackett; Young, Cleverley, Fletcher, Kagawa, Shaw; Zaha, Nani (Hernandez 77)
Kikosi cha Inter Milan: Handanovic (Carrizo 63), Ranocchia, Vidic (Andreolli 72), Juan Jesus, D'Ambrosio, Jonathan, Kuzmanovic (Laxalt 63), Krhin (M'Vila 46), Dodo (Nagatomo 63), Botta (Taider 63), Icardi
0 comments:
Post a Comment