Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Julai 22, 2014, saa 10:13 jioni
KAMA ilivyotegemewa na kushauriwa na watu wengi,
uongozi wa klabu ya Simba chini ya rais Evans Aveva umemsainisha mkataba wa
mwaka mmoja kocha mkuu wa klabu hiyo, Mcroatia, Zdravko Logarusic.
Loga amesaini mkataba huo leo makau makuu ya klabu
ya Simba, mtaa wa Msimbazi, Kariokoo jijini Dar es salaam na kueleza kuwa
kikosi chake kitakuwa bora msimu ujao,
huku lengo kubwa likiwa ni kutwaa ubingwa.
Kitendo cha kupewa kandarasi ya mwaka mmoja
kimemfurahisa Logarusic na kuahidi mambo
mazuri kwa mashabiki na wanachama wa Simba katika mikikimikiki ya ligi kuu
msimuawa 2014/2015 unaotarajia kuanza septemba 20 mwaka huu.
Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange `Kaburu`
ndiye aliongoza zoezi la kumsainisha Loga kandarasi hiyo.
Kaburu alieleza kuwa uongozi umeamua kumpa
majukumu kocha huyo na msalaba uliopo mbele yake ni kuhakikisha Simba
inarudisha heshima kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu bara.
Kwa upande wa kocha msaidizi, Suleiman Abdallah Matola
`Veron`, Kaburu alisema kocha huyo tayari alishasaini mkataba wa miaka miwili
tangu mwezi desema mwaka jana, hivyo hakuna mabadiliko.
Awali kulikuwa na taarifa za uongozi wa Simba
kumtimua Loga, lakini uongozi umeamua kumbakisha kwa kueleza kuwa wameridhishwa
na utendaji wa kazi yake.
Kocha huyo wa zamani wa Gor Mahia ya Kenya
alijiunga na Simba desemba mwaka jana na mechi ya kwanza kuiongozo Simba
ilikuwa ile ya Nani Mtani Jembe ambapo alishinda mabao 3-2.
Hata hivyo alipoanza kushiriki ligi kuu mzunguka
wa pili baada ya kurithi mikoba ya Abdallah Kibadeni, Loga alimaliza msimu kwa
kushika nafasi ya nne.
Mcroatia huyo anasifika kwa kuwa na msimamo mkali
hasa suala la nidhamu kwa wachezaji.
Mara kadhaa wachezaji walidai kocha huyo ni mkali
mno na kuna wakati anashindwa kuwatetea badala yake anawakalipia.
Lakini kwa tamadauni za wachezaji wa Tanzania,
nidhamu ya mpira ni ndogo na kocha anayewasimamia sana anaonekana kuwa mbaya.
0 comments:
Post a Comment