Nyota wa mvuto: Mechi ya fainali ya kombe la dunia katika dimba la Maracana ilikuwa mechi kubwa zaidi katika maisha ya soka ya Lionel Messi.
Imechapishwa Julai 14, 2014, saa 7:58 usiku
MCHEZAJI bora wa dunia mara nne mfululizo, Lionel Messi aliibeba Argentina mabegani mwake katika mchezo wa fainali dhidi ya Ujerumani usiku wa leo na kushuhudia nchi yake ikipigwa bao 1-0 na kukosa ubingwa.
Mamilioni ya Waargentina walifurika Rio de Janeiro wakiwa na matumaini makubwa ya kumuona shujaa wao Messi akikata kiu yao ya kutaka ubingwa, lakini mambo yamekwenda ndivyo sivyo.
Mabeki wa Ujerumani walicheza ngado kwa ngado na Messi na hawakutaka kumuachia hata upenyo.
Mtu wa kukabwa: Messi alikuwa chini ya ulinzi wa wachezaji watatu wa Ujerumani na mpira ulichukuliwa na kiungo fundi Bastian Schweinsteiger.
Mtu pekee: Picha iliyomuonesha Messi akiwa amezingirwa na wachezaji watatu wa Ujerumani, ilikumbusha enzi za gwiji wa pekee nchini Argentina, Diego Maradona ambaye alikuwa chini ya msitu wa wachezaji wa Ubelgiji katika fainali za mwaka 1982.
Messi akichuana kupata mpira baada ya kufanikiwa kuipenya ngome ya ulinzi ya Ujerumani.
Analindwa: Messi akiwa amezingirwa na wachezaji wanne wa Ujerumani , huku akijaribu kutengeneza shambulizi la Argentina.
Haijatimia: Ameshindwa kuandika historia baada ya kushuhudia nchi yake ya Argentina ikipigwa kidude kimoja na Ujerumani.
0 comments:
Post a Comment