Imechapishwa Julai 26, 2014, saa 5:56 asubuhi
PHILIPP
Lahm amefichua siri kuwa alipanga kustaafu soka la kimataifa siku nyingi kabla
ya kutwaa kombe la dunia akiwa nahodha wa Ujerumani.
Nyota
huyo mwenye miaka 30 aliushitua Ulimwengu wa soka baada ya kutangaza maamuzi ya
kustaafu soka la kimataifa baada ya mashindano ya kombe la dunia , huku
ikisalia miaka miwili tu kufikia fainali za mataifa ya Ulaya mwaka 2016.
Lakini
mchezaji huyo wa Ujerumani aliamua kustaafu ili kuwaacha vijana wenye vipaji
waiongoze Ujerumani miaka ijayo.
Lahm
aliuambia mtandao wa Fifa.com kuwa
alikuwa polepole, lakini maamuzi hayo aliyafikia msimu uliopita na alifahamu
kuwa atastaafu baada ya kombe la dunia.
“Nina
furaha kubwa kumaliza soka langu la kimataifa nikibeba kombe la dunia nchini
Brazil. Kwa heshima yangu, ni wakati muafaka wa kuacha soka la kimataifa”.
“Timu
ni nzuri, ina wachezaji wengi wazuri, kuna vijana wadogo wanakuja, acha na wao
wapate nafasi ya kutanua mbawa zao”.
Lahm
alicheza nafasi zote, kama kiungo wa Ulinzi na beki wa kulia wakati wa
mashindano ya kombe la dunia nchini Brazil, lakini aligoma kutajwa kama
mchezaji wa soka aliyekamilika, akitaja mapungufu yake katika sehemu ya
kushoto.
“Naweza
kusema wazi kuwa beki ya kushoto ilikuwa ngumu kucheza na kulitokea krosi
nyingi upande wangu,” alisema. “Kwahiyo sitacheza beki ya kushoto tena.
Madhaifu yangu ya beki ya kulia na kiungo wa ulinzi siwezi kuyataja. Ni juu ya
wapinzani wangu kuyatafuta”.
Nyota
huyo wa Bayern pia alieleza kuwa amekuwa katika mkakati wa kuendeleza soka la
Ujerumani kwa miaka 10 na kuiongoza kutwaa kombe la dunia, akitolewa mfano kuwa
kuna uhusiano mzuri katika timu ya taifa na klabu za Bundesliga.
“Kiukweli
tumenufaika sana na uwezekezaji wa soka la vijana nchini Ujerumani kwa miaka 10
hadi 15,” alisema.
“Kila
klabu ya Bundesliga ina akademi bora, mafunzo ni mazuri na ya kitaalamu na tuna
muda wa kutosha na makocha wenye sifa zote”.
0 comments:
Post a Comment