MARIO Gotze, maisha yanamwendea safi kabisa.
Akitokea kushinda kombe la dunia na nchi yake ya Ujerumani baada ya kufunga bao la dakika za nyongeza, mshambuliaji huyo wa Bayern Munich ameanza likizo akiwa na demu wake kipenzi, Ann-Kathrin Brommel maeneo ya Ibiza.
Wawili hao wamepigwa picha wakifurahia maisha kwenye jua tamu juu ya boti.
Angalau nyota huyo mwenye miaka 22 anastahili kufanya hivyo baada ya kutoa mchango wake wa kuwafanya Ujerumani wawe mabingwa wa dunia nchini Brazil.
Mshindi: Nyota aliyewapa Ujerumani kombe la dunia,Mario Gotze akila bata na mpenzi wake, mwanamitindo, Ann-Kathrin Brommel.
Bata batani!: Gotze na demu wake Brommel wakiwa wametulia juani juu ya boti yao
Muda wa kupunga upepo: Brommel akiwa na basha wake maeneo ya Ibiza
Chukua bebii? Gotze na Brommel wakifurahi pamoja.
Nifunike `hanii`: wawili hao wakila bata baada ya kushinda kombe la dunia majira haya ya kiangazi nchini Brazil
Anajivunia kidume: Brommel yupo likizo na Gotze baada ya kiungo huyo wa Ujerumani kushinda kombe la dunia.
Brommel alionekana uwanjani nchini Brazil baada ya Ujerumani kutwaa `ndoo` ya dunia
Gotze akipumzika maeneo ya Ibiza, Hispania, baada ya kufunga bao zuri lililowapa ubingwa Ujerumani
Gotze akiwa mapumzikoni kabla ya kurudi kuungana na Bayern Munich
Shangwe: Mshindi wa mechi, Gotze alisema wachezaji wa Ujerumani wanatakiwa kufurahia pati `bab kubwa` baada ya kushinda kombe la dunia.
Mabingwa: Gotze na Andre Schurrle wakishangilia ubingwa wa Ujerumani mjini Berlin
0 comments:
Post a Comment