Anatua Bernabeu: Mchezaji wa Colombia aliyeng`ara kombe la dunia na kutwaa tuzo ya mfungaji bora, James Rodriguez anatarajia kujiunga na Real Madrid jumatano.
Imechapishwa Julai 21, 2014, saa 5:56 asubuhi
NYOTA wa kombe la dunia, James Rodriguez, jumatano ya wiki hii atasaini mkataba na Real Madrid utakaogharimu ada ya uhamisho ya paundi milioni 60.
Rodriguez alikuwa nchini Hispania jana jumapili akitokea kwao Colombia na anaelekea katika klabu ya Manaco ambapo ataaga wiki hii kabla ya kurudi tena mjini Madrid kusaini mkataba wa miaka sita.
Rais wa Real Madrid , Florentino Perez yuko Marekani kusini kwa masuala ya kibishara, lakini anarejea wiki hii kuhakikisha kuwa mabingwa hao wa Ulaya wanatumia zaidi ya paundi milioni 80 kwa kumuongeza Rodriguez baada ya kumsajili Toni Kroos kutoka Bayern Munich wiki iliyopita kwa dau la paundi miliobi 20.
Kijana wa dhahabu: Rodriguez anatarajia kusaini mkataba wa miaka sita wiki hii na miamba ya La Liga.
Endelea hivyo hivyo: Real wanaamini nyota huyo mwenye miaka 21 anaweza kuonesha kiwango chake cha kombe la dunia
Uhamisho mkubwa: Rodriguez alikuwa Hispania akitokea Colombia na anakwenda Monaco kuaga.
Msimu uliopita, mchezaji Gareth Bale alisajiliwa kwa dau la paundi milioni 85 ambapo Real Madrid walimuuza Mesut Ozil kwenda Asernal kusaidia kupata hela ya kulipa mkwanja huo.
Usajili huu mwingine mkubwa majira haya ya kiangazi, unaweza kusababisha angalau mchezaji mmoja au watatu kuondoka ili kupata hela.
Manchester United wanaiwinda saini ya Angel Di Maria licha ya msimamo wa kocha Carlo Ancelotti kutaka Muargentina huyo abaki klabuni hapo.
Kuvunja benki ili kumnunua Rodriguez kunaweza kuwashawishi zaidi Madrid kumuuza Sami Khedira na kushuka dau walililotaja la paundi milioni 20.
0 comments:
Post a Comment