KOZI ya ukocha wa mpira wa miguu ya leseni A inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) iliyokuwa ianze kesho (Julai 21 mwaka huu) jijini Dar es Salaam sasa itafanyika mwezi ujao.
Marekebisho hayo yamefanyika kutokana na maelekezo ya CAF ambayo ndiyo itakayosimamia na kuendesha kozi hiyo itakayoshirikisha makocha wenye leseni B za shirikisho hilo.
Tarehe rasmi ya kuanza kozi hiyo itatangazwa wiki ijayo. Mwezi uliopita Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na CAF liliendehsa kozi ya leseni B iliyoshirikisha makocha 29 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF
0 comments:
Post a Comment