Imechapishwa Julai 31, 2014, saa 12:57 jioni
MFARANSA, Herve Renard ameteuliwa
kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ivory Cost leo alhamisi, akirithi mikoba ya
Sabri Lamouchi aliyejiuzulu baada ya nchi hiyo kutolewa katika hatua ya makundi
ya kombe la dunia nchini Brazil.
Renard mwenye miaka 45 alichaguliwa miongoni mwa majina matatu ya
mwisho yaliyowajumuisha kocha wa zamani wa Sporting na Benfica, Jose Manuel De
Jesus kutoka nchini Ureno na Frederic Antonetti, kocha wa zamani wa timu ya
Rennes ya Ufaransa.
Beki huyo wa zamani, aliyeiongoza
Zambia kupata ushindi dhidi ya Ivory Coast kwenye mechi ya fainali ya mataifa
ya Afrika mwaka 2012 nchini Gabon, amepewa kazi ya kuhakikisha Tembo hao
wanafuzu fainali za AFCON 2015 nchini Morocco.
Rais wa chama cha soka nchini Ivory
Coast alisema Renard ndiye mwenye mpango mzuri kwa nchi hiyo, na hata mshahara
wake aliotaja unalipika, hivyo ndiye aliyestahili.
Renard anakabiliwa na changamoto ya
kuitengeneza timu upya baada ya wachezaji wengi kutupwa na umri.
Pia mashabiki na vyombo vya habari
vimekuwa vikiiponda timu hiyo, hivyo ni kazi kwake kuiweka sawa.
Kocha huyu amesaini mkataba wa miaka
mwiwi ambao unaweza kuongezwa kama atafanya vizuri,na hii kwa mujibu wa rais wa
chama cha soka nchini Ivory Coast, Augustin Sidy Diallo.
0 comments:
Post a Comment