Imechapishwa Julai 22, 2014, saa 12:24 jioni
KLABU
ya Yanga imembwaga mshambuliaji wake Mganda, Khamis Kiiza ‘Diego wa Kampala’ baada
ya kusajiliwa kwa Wabrazil wawili, Andrey Coutinho na Geilson Santos Santana
`Jaja`.
Baada
ya Jaja kusaini mkataba wa miaka miwili jana makao makuu ya klabu ya Yanga,
kulikuwa na utata ni mchezaji gani atapigwa chini kati ya Kiiza na Emmanuel Anord
Okwi.
Awali
ujio wa Jaja ulielezwa kuwaweka kitimoto Kiiza na Okwi, huku mmojawapo
akitakiwa kutolewa kafara.
Taarifa
za uhakika ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba kocha Maximo amependekeza
kuachwa kwa Kiiza kutokana na ripoti iliyoachwa na Hans Van Der Pluijm.
Mzigo
huo uliofuatwa chini ya kapeti unasema kuwa Pluijm katika ripoti yake
aliyowasilisha kwa viongozi baada ya kumalizika kwa msimu uliopita, alisema ili
Emmanuel Okwi acheze Yanga sc, lazima Kiiza aondolewe.
Kwa
kuzingatia mapendekezo hayo, Maximo amefuata ushauri huo na sasa Kiiza rasmi
anaondoka Jangwani.
Katika
hatua nyingine, imeelezwa na chanzo cha uhakika kuwa Maximo amewabana viongozi
wa Yanga akiwataka wajenge uwanja wa mazoezi wa Kaunda ili kuepukana na adhaa
anayoipata.
Maximo
amewakazia na amesema hakuna jinsi, lazima uwanja huo ujengwe muda huu.
Pia
amewataka viongozi kuboresha vyumba vya jengo la Jangwani ili wachezaji wote
waishe pale.
Taarifa
zinasema, Maximo amesema haiwezekani timu kukaa saa mbili kwenye foleni
inapoelekea uwanjani na kurudi kambini.
Kwa
mazingira hayo anataka wachezaji wake wakae makao makuu ya Yanga, mitaa ya
Twiga na Jangwani, halafu uwanja wa Kaunda
ujengwe.
Mbrazil,
Marcio Maximo anafahamika kwa kuwa na msimamo mkali katika mambo yake.
0 comments:
Post a Comment