Anaonekana kuvutia: Mshambuliaji, Joel Campbell amejiunga na wachezaji wenzake wa Arsenal katika kambi ya Austria.
Imechapishwa Julai 30, 2014, saa 1:31 jioni
Joel Campbell amepigwa picha akifanya mazoezi kwa mara ya kwanza na kikosi cha Asernal.
Nyota huyo mwenye miaka 22 alishiriki mazoezi hayo huko Austria, ambapo klabu imeweka kambi ya siku nne kabla ya kurudi kuwa mwenyeji wa kombe la Emirates.
Katika kombe hilo, Asernal itacheza dhidi ya Benfica na Monoca.
Msimu uliopita Campbell alionesha kiwango kizuri akiwa na mabingwa wa Ugiriki , Olympiacos, akifunga mabao 7 yakiwemo mawili dhidi ya Manchester United katika hatua ya 16 ya ligi ya mabingwa Ulaya.
Arsene Wenger akimtazama kwa umakini Joel Campbell nchini Austria
Ujuzi: Campbell anatarajia kuonesha ujuzi wake akiwa na Asernal msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment