Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Mtandao
Imechapishwa Julai 23, 2014, saa 3:38 usiku
KULIKUWA na maswali mengi zaidi kuliko majibu kufuatia James Rodriguez kujiunga na Real Madrid kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 80 sawa na paundi milioni 60 kutokea klabu ya Manaco.
Wapi Mkolombia huyo atacheza? anastahili ada kama hiyo ya uhamisho?, kweli
Real Madrid inamhitaji yeye?
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez hana
wasiwasi. Kiwango kikubwa alichoonesha katika fainali za kombe la dunia akiwa
na taifa lake ndio sababu ya Real kumsajili majira haya ya kiangazi.
Usajili huo umekuwa mkubwa zaidi ya Toni Kroos
aliyesaini mkataba wa miaka sita na mabingwa hao wa Ulaya wiki iliyopita.
Licha ya kipaji alichonacho Rodriguez, mashabiki
wa Real Madrid wamebaki wakishangaa kama kweli mchezaji huyo mpya atakayevalia
jezi namba 10 atang’ara na klabu kama alivyofanya Brazil akiwa na Colombia.
Mchezaji huyo wa zamani wa Porto alitwaa tuzo ya
mfungaji bora wa kombe la dunia kwa kufunga magoli sita na kuiongoza Colombia
mpaka hatua ya robo fainali.
Pia aling’ara akiwa na klabu yake ya Monaco katika
michuano ya Ligue 1 msimu uliopita, lakini amekuja katika macho ya watu wengi
zaidi majira haya ya kiangazi.
Wakati Kroos akiwasili kwa dau linaloingia mara
tatu kwa lile la Rodriguez baada ya kushinda kombe la dunia, nyota huyo kijana
ameingia katika orodha ya wachezaji ghali zaidi duniani akishika nafasi ya nne
baada ya Gareth Bale, Cristiano Ronaldo na Luis Suarez.
Kuwa na kipaji, hakuna wasiwasi, lakini kuna vitu
vingi vya kuthibitisha.
Je, mchezaji huyo wa Monaco na Porto anaweza
kuonesha vitu vyake Real Madrid mbele ya wachezaji wengi nyota?
Kitu cha kwanza: Mchezaji huyu mwenye miaka 23 ana
kipaji. Kucheza nyuma ya mshambuliaji akiwa na Colombia nchini Brazil
kulimfanya aonesha uwezo mkubwa akifunga bao zuri lililojadiliwa kuwa miongoni
mwa mabao bora.
Alionekana kuwa mtulivu kwenye michuano hii
mikubwa zaidi duniani. Pia alipiga pasi za mwisho za mabao 12 katika ligi ya
Ufaransa msimu uliopita na alifunga
mabao 9 akiwa na Monaco na alitajwa kuwa mchezaji bora wa timu hiyo.
Madrid wamemsajili mchezaji anayeweza kwenda
katika kiwango cha juu zaidi.
Atacheza wapi Bernabeu? Wakati huu Kroos akiwa
amejiunga na mabingwa hao wa ulaya. Angel di Maria na Sami Khedira wanaweza
kuondoka klabuni hapo majira haya ya kiangazi, lakini bado swali linabaki kama
Mcolombia huyo ataweza kuingia katika kikosi cha kwanza cha Real Madrid.
Siasa zinaweza kutawala hili. Baada ya Cristiano
Ronaldo na Gareth Bale, Rodriguez atakuwa mchezaji ghali zaidi kwenye kikosi
cha Real Madrid na Perez hatapenda kuona fedha kubwa kiasi hicho zinakaa
benchi.
Kocha Carlo Ancelotti atalamizika kumchezesha
mchezaji huyo hata kama anapenda au hapendi.
Lakini katika jicho la ufundi, Rodriguez hawezi
kuanza katika kikosi cha kwanza kwa wakati wote.
Nyota huyo anapenda kucheza nyuma ya mshambuliaji,
kwa mazingira hayo atakuwa Karim Benzema.
Lakini Cristiano Ronaldo na Garthe Bale wote huwa
wanaanza, kuongezeka kwa Rodriguez kutamfanya Ancelotti aanzishe kikosi
kitakachoshambulia zaidi. Huo ndio utamaduni wa Real Madrid, wengine wanasema
kuwa na usawa kikosini sio suala muhimu.
Viungo wawili wa kati wataachwa kulinda safu ya
ulinzi na kuunganisha safu ya ushambuliaji, lakini msimu uliopita, Real Madrid
walikuwa wanayumba katika safu ya kiungo wanapocheza na timu kubwa. Tatizo
yawezekana lilikuwa katika mfumo wa kwanza wa 4-2-3-1 uliokuwa unawapa nafasi
wachezaji wote nyota.
Badala yake, mfumo wa 4-3-3 unaoogopwa zaidi wa
`BBC`, Bale, Benzema na Cristiano Ronaldo utatumika tena, katikati watakuwa
watatu, Kroos, Xabi Alonso na Luka Modrid , huku Rodriguez akiwa benchi, na unaonekana
kukamilika.
Wachezaji wote watatu wa katikati wanaweza
kusaidia ulinzi na wanaweza kucheza kama viungo wa ulinzi. Kuwapanga wawili na
kumuingiza Rodriguez kutaifanya timu ishambulie zaidi na haitakuwa busara kwa
safu ya ulinzi.
Kwahiyo Rodriguez atafanya nini? Ancelotti
alionekana kumuongeza Isco katika safu ya kiungo cha kati msimu uliopita.
Kitendo kilichomfanya nyota huyo ashindwe kuonekana vizuri na kuachwa katika
kikosi cha timu ya taifa ya Hispania.
Rodriguez anaweza kucheza vizuri nafasi hiyo na
itakuwa nzuri zaidi baada ya Alvaro Morata kuondoka na kujiunga na Juventus majira haya
ya kiangazi. Kuna uwezekano wa kucheza na Ancelotti ataweza kumtumia.
Ada kubwa ya uhamisho haijamsaidia Rodriguez; ada
kubwa kazi hizo hazifanyi kazi. Kunakuwa na presha kubwa kwa wachezaji wa aina
hiyo Real Madrid, lakini ada hiyo ambayo ni ya nne kwa ukubwa katika historia
ya uhamisho wa wachezaji itaongeza majukumu zaidi kwenye mabega ya mshambuliaji
huyo.
Haijulikani kama atamudu ada yake au atashindwa
kama walivyoshindwa wachezaji wenzake Isco na Asier Illarramendi, waliowasili
Bernabeu kwa ada kubwa msimu uliopita, lakini walishindwa kutamba na kubaki
kukalia benchi.
Mambo yanavyoonekana, Usajili wa Rodriguez
unaonekana kuwa wa kujifurahisha na sio lazima. Ni juu yake kuwathibitishia
watu uwezo wake.
0 comments:
Post a Comment