Imechapishwa Julai 30, 2014, saa 3:24 asubuhi
IVORY Coast itatangaza jina la kocha mpya wa timu
ya taifa ya nchi hiyo kesho alhamisi mchana, kwa mujibu wa shirikisho la soka.
Shirikisho lilisema kwamba, usaili wa mwisho kwa
majina matatu yaliyosalia unakamilika
leo jumatano mjini Abidjaan, mji mkuu wa nchi hiyo na mji mkuu wa kibiashara.
Mfaransa Herve Renard anaonekana kuwa ndiye
atashinda nafasi hiyo, kwa mujibu wa vyanzo vya mtandao wa michezo wa Supersport.com ndani ya shirikisho la
nchi hiyo.
Beki huyo wa zamani mwenye miaka 45, aliyeiongoza
Zambia kutwaa ubingwa wa kombe la mataifa ya Afrika, AFCON 2012, anafurahia
kuungwa mkono na viongozi wakubwa wa soka na wizara ya michezo ya Ivory Coast.
Hata hivyo, kocha wa zamani wa Sporting na
Benfica, Jose Manuel De Jesus kutoka Ureno naye anaonekana kupewa nafasi ya juu
kutokana na uzoefu wake mkubwa kwa soka la ulaya. Lakini hajawahi kuongoza timu
ya taifa, kitendo ambacho vyanzo vinaeleza kuwa kitamuangusha katika nafasi
hiyo.
Herve Renard anapewa nafasi kubwa ya kuwa kocha mpya wa Ivory Coast
Mfaransa mwingine, Frederic Antonetti,
aliyeifundisha Rennes, pia anapewa nafasi miongoni mwa majina matatu ya mwisho
yaliyotolewa wiki iliyopita na shirikisho la soka. Ingawa hana uzoefu wa kufundisha
timu ya taifa, lakini ujuzi wake wa kuendeleza vipaji unampa nafasi ya
kuchaguliwa.
Zaidi ya makocha 37 waliomba kazi hiyo, akiwemo
kocha wa zamani wa Tembo hao, Francois Zahoui. Katika orodha hiyo, majina
yalipunguzwa mpaka matano na baada ya usaili wa pili yakabakia matatu ambayo
yanasailiwa kwa mara ya mwisho.
Kocha mpya atapewa kazi ya kuiandaa timu kwa ajili
ya kufuzu kucheza michuano ya Afrika mwaka 2015 nchini Morocco.
0 comments:
Post a Comment