Na Baraka Mbolembole
Azam FC ilianzishwa mwaka 2007, lakini timu hiyo
ilikuwepo tangu mwaka 2004 ikiwa chini ya wafanyakazi wa kiwanda . Awali timu
hiyo ilikuwa ikifahamika kama Mzizima FC, ingawa ilianzishwa kwa lengo la kuwafanya wafanyakizi kujiweka vizuri
kiafya, timu hiyo ilikuwa ikishiriki katika ligi daraja la Tatu, Manispaa ya
Ilala hadi mfumo huo wa madaraja ulipoondolewa mwishoni mwa mwaka 2005.
Wazo la Abubakary Bakhressa kuanzisha timu
kabambgi daraja la Tatu, Manispaa ya Ilala hadi mfumo huo wa madaraja
ulipoondolewa mwishoni mwa mwaka 2005.
Wazo la Abubakary Bakhressa kuanzisha timu
kabambeyo ilikuwa ikihusisha mabingwa wa Mikoa. Mara baada ya kupanda ligi kuu,
Azam FC ilifanya usajili wa wachezaji nyo walioshika nafasi ya pili, na
Simba ubingwa.
Msimu wake wan ne katika ligi kuu timu hyo ilifanikiwa kumaliza katika nafasi ya pili
nyuma ya waliokuwa mabingwa Simba SC kwa tofafauti ya pointi mbili. Baada ya
kuipiga kumbo Mtibwa Sugar katika misimu miwili ya nyuma katika nafasi ya tatu,
safari hii Azam iliwaondoa Yanga na kuwa miongoni mwa timu mbili za juu.
Baada ya kupiga hatua hiyo na kupata nafasi ya
kuiwakilisha nchini katika michuano ya Kimataifa, Azam iliendelea kupandisha
ubora wake wa kiuchezaji na kimipango na kufanikiwa kwa mara nyingine kumaliza
katika nafasi ya pili katika msimu wa 2012/13 nyuma ya Yanga ambao walitwaa
ubingwa huo. Simba ilitupwa nje ya timu mbili za juu.
MSIMU WA MAFANIKIO
AZAM FC ilitwaa ubingwa wake wa kwanza wa ligi kuu
Tanzania Bara katika msimu wa 2013/14 ukiwa ni msimu wao wa sita tangu
walipopanda ligi kuu. Ni mafanikio makubwa lakini kote huko kuna njia ngumu
ambayo wamepitia. “ Msimu wa 2014/14 ndiyo msimu wetu bora kwa kuwa
tulifanikiwa katika malengo yetu” anasema meneja wa timu hiyo. Jemedari Daid
“ Tulikuwa na melengo mawli, Kwanza ilikuwa ni
kuhakikisha tunafanya vizuri na walau
kufika robo fainali katika michuano ya kombe la shirikisho baani Afrika, na
lengo la Pili ilikuwa ni kutwaa ubingwa wa ligi kuu. Tulifanikiwa katika lengo
la Pili na tulitolewa mapema katika michuano ya Shirikisho na timu ya
Ferreviaro Beira ya Msumbiji. Tulishinda mchezo wa kwanza nyumbani kwa bao 1-0
na tukafungwa mabao 2-0 ugenini. Mara baada ya kutolewa katika michuano hiyo
tulielekeza nguvu zetu katika ligi kuu na tulifanikiwa kutwaa ubingwa”
Swali; Azam iliwezaje kutwaa ubingwa”
JEMEDARI; Kuwa bingwa hakukuja tu, tulikuwa na ‘
plan’ ya muda mrefu kidogo. Baada ya kumaliza katika nafasi ya Tatu kwa misimu
miwili ( 2009/10-2010/11) na kumaliza katika nafasi ya Pili mara mbili ( 2011/12-2012/13, tuliweka malengo ya
kuhakikisha tunatwaa ubingwa msimu uliofuata. Nachoweza kusema ni kwamba
Mwalimu, Stewart Hall amechangia kwa asilimia kubwa ubingwa wetu msimu
uliopita. Nampa asilimia 65 hadi 70 kuwa alifanikisha ubingwa . Ukizungumza wa
weledi, timu inapitia sehemu mbili muhimu ili kuelekea katika ubingwa.
Kwanza, ni kwenye usajili, Pili ni kwenye
maandaalizi. Ukifeli katika usajili na maandalizi huwezi kuwa bingwa, Mwalimu,
Hall ndiye aliyeshiriki kwa asilimia kubwa katika kusajili timu na ni yeye
aliyefanya maandalizi mazuri. Kabla ya msimu kuanza Mwalimu, Stewart alikaa na
wachezaji wote pamoja na viongozi wa klabu na akawaeleza nia yeke ya kutwaa
ubingwa.
Tarehe 9, julai, 2013 kulifanyika kikao kati ya
benchi la ufundi na wachezaji wote , ilikuwa ni kabla ya mchezo wa kirafiki
dhidi ya timu ya Kombaini ya Polisi Tanzania katika mchezo wa kirafiki ndani ya
uwanja wa Taifa. Nakumbuka mchezo huo tulishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na
Ladson Kakolaki Hall aliwaambia kwa nini wanataka kuwa mabingwa. Ni sehemu zipi
ambazo tuzifanyie kazi ili kuwa mabingwa.
SWALI; Mlichukuliaje changamoto ya misimu
iliyopita?
JEMEDARI;
Msimu ambao Simba SC walikuwa mabingwa tulizidiwa kwa pointi sita, na
msimu uliofuata ambao Yanga walikuwa mabingwa tulikuwa nyuma kwa pointi sita
pia, lakini tulikuwa na pointi 56 katika
michezo yote ya msimu, Hall akatuambia kuwa ili kuwa bingwa wa ligi kuu ni
lazima uwe na pointi 60 hadi 61 kwa hiyo alisema tuongeze point inane katikac
zile 56 na tutakuwa mabingwa. Tunawezaje kupata pointi hizo?
Stewart aliwaelekeza viongozi na kuwaambia kuwa
kuna maeneo ni lazima yaboreshwe. Kwanza ni ‘ U-proffesionalsm’ ni lazima
tuongeze kwa asilimia tano, ‘ fitness’
tuongeze pia kwa asilimia tano na akawaambia wachezaji kuwa eneo lingine
ni katika ‘ ufundi na mbinu’ alihitaji
pia tuongeze kwa asilimia tano.
Katika ‘ Fitness’
alishauri tumuajiri mtu ambaye ana uwezo na mtaalamu wa idara hiyo na
akaajiliwa Mtu sahihi kutoka nje ya nje. Wachezaji wamekuwa na vipindi maalumu
katika siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa kulikuwa na ‘ section’ moja moja ya
gym ili kuongeza nguvu kwa wachezaji. Aliwashauri wachezaji wazawa kucheza
mpira kama wachezaji wa kulipwa na kuachana na mambo ambayo yatawafanya kuwa
nje ya kazi yao. Aliwambia anafahamu wanaishi nyumbani lakini wanapaswa kupunguza sababu ambazo
zinawafanya wawe nje ya timu kama sababu za ‘ mtoto au mzazi kuumwa ‘ .
Aliwaambia watambue kuwa wapo kazini na kuna watu wanawategemea. Alitaka
wachezaji wote wasikose mazoezini.
Aliwataka wachezaji waboreshe ufundi wao binafsi,
pia aliwataka kufuatilia mafundisho na melekezo yote ya kiufundi ambayo
watakuwa wakipewa. Hivyo ukiunganisha asilimia hizo 15 na kuongeza pale
tulipokuwa tumeishia katika misimu miwili ya mwisho tungeweza kabisa kupata
pointi hizo nane hadi kumi na kutwaa ubingwa.
SWALI; Je,
ujumbe huo ulifika ipasavyo kwa wachezaji?
JEMEDARI; Tunashukuru wachezaji walimuelewa japo
kuwa mwanzoni wakati wa maandalizi kuna wanachezaji walionekana kusuasua,
tulianza maandalizi Juni 24, 2013 ambayo yaliwahusisha wale wachezaji wasiokuwa
na majukumu yoyote katika timu za Taifa. Wale wachezaji ambao walikuwa katika
timu za Taifa walipewa wiki mbili za mapumziko
Wachezaji wa kigeni wao walipewa ruhusa wiki moja
kabla ya wachezaji kuondoka. Nakumbuka mchezo wa mwisho wa ligi ambao tulicheza
Arusha ( dhidi ya JKT Oljoro msimu wa 2012/2013) wachezaji wote wan je walikuwa
tayari wamepewa ruhusa ya kurudi nyumbani kwao. Hivyo walitakiwa kuwahi
maandalizi ya msimu mpya baada ya wiki moja, hivyo katika wiki ya pili wote
walikuwa tayari wamewasili.
Baada ya hapo tulicheza michezo mingi ya kujipima
nguvu katika uwanja wetu wa Azam Complex Chamanzi. Tulianza kucheza michezo ya
kirafiki na timu za kawaida, tulicheza na African Lyon mara mbili, timu yetu ya
Pili, kabla ya tarehe 4, agosti kusafiri kwenda Afrika Kusini kucheza michezo
minne ya kujiandaa na msimu. Nachoweza kusema ‘ pre-season’ yetu yote ilikuwa
kule.
Wakati tupo kule Mwalimu alipendekeza mtu mmoja
anayeitwa Taylers ambaye alisafiri kutoka London, England na kuunga nasi tukiwa
kule. Mechi yetu ya kwanza tulicheza na
Kaizer Chiefs jijini , J,burg na tulipoteza kwa magoli 3-0.
SWALI; Kuna kitu ambacho mlijifunza baada ya
mchezo huo?
JEMEDARI; Mechi ile ilitufunza mambo mengi,
ilionesha tofauti kubwa kati yetu na wao. Baada ya mchezo ule tulikwenda katika
uwanja wa mazoezi na wachezaji wote na kila mchezaji alikiri kuwa wenzetu wapo
mbali zaidi ya tulipo sisi, unajua wachezaji nao ni binadamu hivyo baada ya
kuona wamepata kuwa washindi wa pili mara mbili katika ligi ya nyumbani wengine
wanaweza kujiona ni wachezaji wakubwa. Lakini baada ya kipigo kile kutoka kwa
Kaizer kila mmoja aliona udhaifu wake, ilikuwa mechi ambayo Kaizer walitumia
vijana wa timu yao ya Pili kwa asilimia kubwa kuliko wale wa kikosi cha kwanza.
Walitumia wachezaji wane ambao hawakuwa wakipata
nafasi sana katika michezo ya ligi kuu ya Afrika Kusini, lakini kile ambacho
walikifanya na tulichokishuhudia kila mtu kila mpa nafasi ya kujiuliza mara
mbili mbili. Tulijiuliza ni kweli ni ‘ sisi washindi wa pili mara mbili
mfululizo katika ligi kuu ya Tanzania Bara’ au? Ni, kweli tulikuwa tayari
kufika robo fainali ya michuano ya CAF?. Kila mmoja alishtuka na kujiuliza
maswali mengi.
Kitu kizuri tulikwenda pale kujifunza na kila
mchezaji alikubali kuwa kiwango chetu kipo chini. Tulijua kuwa mechi zote
zitakazofuata zitakuwa kama ile ( dhidi ya Kaizer) lakini bahati nzuri baada ya
siku mbili tukacheza na Mamelod Sundown ( mabingwa wa mwaka jana wa PLS)
Tukacheza nao katika uwanja wao wa mazoezi tukafanikiwa kuwafunga kwa bao 1-0
ambalo lilifungwa na mshambulizi, Gaudensi Mwaikimba.
Kocha wa Sundown, Pitso Mosimane, na meneja wa
timu hiyo Peter Ndlovu ( mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Zimbabwe) Walifanya mahojiano na sisi na kutuuuliza
tupo katika nafasi gani katika ligi kuu, tukawaambia kuwa sisi ni washindi wa
pili mara mbili mfululizo. Wakatuambia kuwa kama tutaendelea kucheza kama
ilivyokuwa katika mchezo ule dhidi yao basi tungekuwa na nafasi kubwa ya kuwa
mabingwa katika ligi . Kitu ambacho kilikuja kutokea kweli baadae.
Mechi ya tatu tulicheza na Orlando Pirates ambao
walikuwa wakicheza klabu bingwa Afrika hivyo walileta wachezaji mchanganyiko
kutoka timu ya kwanza na ile ya pili. Tulipoteza mchezo hule kwa mabao 2-1,
mechi ile ilikuwa ngumu sana lakini tayari tulikuwa tumeanza kuzoea kucheza
dhidi ya timu za Afrika Kusini. Mechi ile nakumbuka ilitugharimu sana kwani
tulicheza katika hali ya baridi kali na mvua kubwa ambayo ilinyesha usiku wa
kuamkia siku ya mchezo ambao tulicheza asubuhi.
Baada ya mchezo huo tulikwenda Soweto kucheza na
Maroka Swallows tukafungwa goli 1-0 lakini ni mechi ambayo tuliona uwezo wa
golikipa wetu mdogo, Aishi Manula, licha ya Swallows kufunga goli moja kijana
huyo alifanya kazi kubwa sana. Mechi mbili alicheza Mwadini Ally kipa wetu
mzoefu na mbili alicheza Aishi na kutokana na kiwango alichokionesha Aishi,
Mwalimu, Stewart aliona hakuna sababu ya kumpanga Mwadini katika mchezo wetu wa
ufunguzi wa msimu ‘ Ngao ya Jamii’ dhidi ya Yanga ambao ulichezwa tarehe 17,
agosti, 2013.
Mwalimu alisema kuwa Mwadini alikuwa amepita
kipindi kigumu sana, kwani tangu alipocheza mchezo wa mwisho wa ligi kuu msimu
wa 2012/13 hakuwa amecheza mchezo wowote katika timu ya Taifa, hivyo kutokana
na Mwadini kuonekana kukosa ‘ match fitness’ Mwalimu alifanya maamuzi ya
kumtumia, Aishi katika mchezo dhidi ya Yanga.
SWALI; Baada ya kurudi nchini nini kiliendelea?
JEMEDARI; Tulicheza mchezo wa kwanza dhidi ya
Yanga katika Ngao ya Jamii na kufungwa kwa goli 1-0. Tulianza ligi kwa kucheza
na Mtibwa Sugar na kulazishwa sare ya kufungana bao 1-1 katika uwanja wa
Manungu, tukaenda Tabora kucheza na Rhino na kushinda kwa mabao 2-0 na tukaenda
Bukoba kucheza na Kagera Sugar, na kutoka sare ya kufunga bao 1-1. Na kabla ya
kupisha kambi ya timu ya Taifa tulicheza na Ashanti United na kupata sare ya
bao 1-1.
Hayakuwa matokeo mazuri sana kutokana na
maandalizi ambayo tuliyafanya. Tuliamini namna timu nyingine zilivyokuwa
zimejiandaa na maandalizi tuliyokuwa tumeyafanya kwa upande wetu tulistahili
kupata matokeo bora zaidi ya hayo. Tulifikiri mechi ya Ashanti ilikuwa ni
lazima tupate matokeo baada ya kushindwa kufanya hivyo dhidi ya Mtibwa na
Kagera katika viwanja vya ugenini. Mchezo dhidi ya Ashanti ambao ulikuwa wa
kwanza katika uwanja uwanja wa nyumbani, Azam Complex Chamanzi, ulituongezea
machungu zaidi.
Hali haikuwa nzuri sana na tukaanza kupata
wasiwasi, siyo kutokana na matokeo tu ya uwanjani bali namna timu ilivyokuwa
ikicheza tulipatwa na wasiwasi kwa kuwa mchezo uliokuwa ukifuata ulikuwa dhidi
ya Yanga ambao tayari walikuwa wametufunga katika mchezo wa Ngao ya Jamii,
lakini tukaona baada ya pale kuna unaliza wa kuwatumia wachezaji wa timu ya
Pili.
Kwa mara ya kwanza katika kikosi cha wachezaji 18
kulikuwa na wachezaji watatu wa Academy yetu. Farid Mussa Shaa. Joseph Kimwaga
ambaye alifunga goli la ushindi katika dakika ya mwisho ya mchezo, na Leonard Luis Mlingila. Katika mchezo ule
Farid alianza kama winga wa kushoto na wengine walikuwa katika benchi. fArid
alifanya vizuri na ndiye alitoa krosi ya goli la kwanza, alipotoka na kumpisha Kimwaga ambaye alikuta matokeo
yakiwa sare ya mabao 2-2 alifunga bao zuri la ushindi. Tukaanza kuwaamini
vijana wa timu yetu ya Pili na kuona tuna hadhina kubwa. Tulitumia vijana zaidi
ya saba kwa msimu mzima.
Gabriel Michael ambaye alikuwa mchezaji wa
kutegemewa katika raundi ya pili kama mlinzi wa kushoto, Kelvin Friday na
Yahaya Abbas ni vijana wengine ambao walipandishwa katika timu ya kwanza kutoka
katika Academy na walitoa mchango mkubwa kwa timu.
MATOKEO
YA AZAM FC MZUNGUKO WA KWANZA
Azam ilitwaa ubingwa baada ya kufikisha
pointi 62 katika mi8chezo 26, walianza msimu kwa sare mfulizo dhidi ya Mtibwa
Sugar katika uwanja wa Manungu, Turiani. Katika mchezo huo wa kwanza, Azam
ikiwa chini ya kocha Stewart Hall ililazimisha sare ya kufungana goli 1-1 goli
la vAzam katika mchezo huo lilifungwa na mlinzi, Aggrey Morris, hihi ilikuwa
ni septemba 24 na siku nne baadae,
waliichapa Rhino Rangers kwa magoli 2-0 katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi,
Tabora. Magoli ya Kipre Tcheche yaliwapatia ushindi wao wa kwanza wa msimu tena
wakiwa ugenini.
Walianza mwezi oktoba kwa sare ugenini
dhidi ya timu ngumu ya Kagera Sugar katika uwanja wa Kaitaba, Bukoba. Sare ya
kufungana goli 1-1 ilionekana ni kama timu hiyo haina uwezo wa kutwaa ubingwa
lakini ilikuja kuonesha umuhimu wake wakati ligi ikiwa ukingoni huku timu
zikipishana pointi chache. Pointi moja ya Kagera ilikuwa muhimu. Hamis Mcha ‘
Vialli’ ndiye alikuwa mkombozi katika mchezo huu baada ya kufuta goli la Themi
Felix na kuisawazishia timu yake
Katika mchezo wa kwanza ndani ya uwanja
wake wa nyumbani, Azam ilijikuta ikilazimishwa sare na Ashanti United ambao
walikuwa wamepoteza michezo yote mitatu ya mwanzo. Mlinzi wa United na mchezaji
wa zamani wa Azam, Tumba Sued aliswazisha goli la Kipre Tcheche dakika tano kabla ya kumalizika
kwa mchezo na kufanya timu hizo kufungana goli 1-1 . Hali hiyo ilianza kutia
shaka kama ni kweli timu hiyo ingeweza kumaliza katika nafasi mbili za juu
achilia mbali kutwaa ubingwa. Hakika mwezi, oktoba ulikuwa mgumu sana kwa timu
hiyo kwa kuwa haikupata ushindi wowote katika michezo minne mfululizo.
Baada ya sare dhidi ya Kagera Sugar na
Ashanti United, Azam ilisafiri hadi jijini, Mbeya kuikabili Tanzania Prisons na
kwanyingine Tcheche akawa mwokozi wa timu hiyo pale alipofunga goli pekee la
Azam katika sare ya kufungana goli 1-1. Azam walibanwa na ratiba katika raundi
ya kwanza nap engine jambo hilo liliwafanya kupata matokeo ambayo yalionekana
mabaya. Walikwenda jijini, Tanga na kulazisha suluhu-tasa dhidi ya Coastal
Union.
Baada ya kuambulia pointi nne katika
michezo minne ya mwezi, oktoba, Azam ilirejea katika uwanja wake wa Azam
Complex Chamanzi, na kuichapa timu ya JKT Mgambo ya Tanga kwa magoli 2-0.
Washambuliaji waliokuwa majeruhi, John Bocco na Mganda, Brian Omony walifunga
magoli yao ya kwanza katika msimu wa 2013/14 na kuisaidia timu yao kuibuka na
ushindi wa pili wa msimu katika michezo saba.
Kiungo, Mkenya, Humphrey Mieno, mlinzi,
Erasto Nyoni na kiungo Salum Abubakary ‘ Sure Boy’ kila mmoja alifunga goli
lake la kwanza la msimu wakati Azam ilipoichapa JKT Ruvu kwa magoli 3-0 katika
uwanja wa Azam Complex Chamanzi. Mwezi novemba ulikuwa mzuri kwa kikosi cha
Hall, na walikwenda Arusha na kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya JKT
Oljoro, mshambulizi Bocco ndiye alikuwa mfuingaji wa goli pekee katika mchezo
huo.
Kwa mara nyingine, Bocco na Mcha
wakaibuka katika orodha ya wafungaji wakati walipoisadia timu yao kuichapa
Simba SC kwa magoli 2-1. Kitendo cha kuifunga Simba ilikuwa ni dalili za timu
hiyo kuonesha ipo tayari kupambana kuwania taji japokuwa hakufanya vizuri
katika michezo mitano siku za nyuma.
Wakaichapa Yanga SC isivyotarajiwa kwa
magoli 3-2, Kipre, Mcha, na chipukizi Joseph Kimwaga walikuwa wafungaji
wamagoli ya Azam katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua. Bocco, Erasto, na Sure Boy walikuwa wafungaji
wa magoli ya Azam wakati ilipoichapa Ruvu Shooting kwa magoli 3-0 katika uwanja
wa Azam Complex Chamanzi. Azam FC ilimaliza mzunguko wa kwanza kwa kulazimishwa
sare ya ‘ajabu’ katika uwanja wa nyumbani dhidi ya Mbeya City. Azam ililazishwa
sare ya kufungana magoli 3-3, Mcha, Tcheche na Mieno walikuwa wafungaji wa Azam
wakati, Mwigane Yeya alifunga magoli yote ya City siku hiyo . Katika michezo 13
walikusanya pointi 26.
MATOKEO MZUNGUKO WA PILI
Azam FC, ilianza duru la pili la ligi
kuu Tanzania Bara kwa ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya timu ya Mtibwa
Sugar. Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na mshambulizi, Kipre Tcheche.
Wakashinda michezo mingine mitatu kati ya minne waliyocheza katika mwezi wa
pili,
baada ya kuifunga Mtibwa, walizichapa timu za JKT Oljoro, Kagera Sugar katika uwanja wa Chamanzi. Kipre baada ya kufunga katika michezo miwili dhidi ya Mtibwa na Rangers, safari hii ni Brian Omony kiungo-mshambulizi wa kimataifa wa Uganda aliyefunga mara mbili, kinda Kelvin Friday akafunga bao lake la kwanza katika ligi kuu, na kiungo Jabir Aziz akahitimisha ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kagera.
Azam ilishuhudia Tanzania Prisons
ikipata sare ya kufungana mabao 2-2.
Aggrey Morris katkulazimishwa sare, AzamFC iliibuka na ushindi
mwingine ' mnono' wa mabao 4-0 mbele
ya Ashanti United.. Aggrey, na patna wake katika safu ya ulinzi, Said Mourad
walifunga bao moja kila mmoja na mshambulizi, Gaudensi Mwaikimba akafunga
mara mbili katika mchezo huo.
Kipre
alifunga bao moja, Friday alifunga bao lingine moja, nahodha John
Bocco akafunga mara mbili katika mchezo huo dhidi ya Coastal Union. Baada ya
mchezo huo Azam ilikutana na waliokuwa mabingwa watetezi wa taji, Yanga
katika uwanja wa Taifa. Na kulazimisha sare ya bao 1-1, kinda Friday alisawazisha
dakika tano kabla ya mchezo kumalizika na kulinda uongozi wa tofauti ya
pointi nne baina yao na Yanga.
Wakaifunga Simba kwa mabao 2-1. Mabao
yote yakifungwa na Kipre Tcheche. Walikwenda Arusha kucheza na JKT Oljoro na
kiungo wa pembeni Hamis Mcha alifunga bao pekee katika ushindi wa bao 1-0.
Baada ya mchezo huo wa Arusha, ligi kuu ilikuwa imesalia na michezo mitatu na
Azam waloikwenda Mlandizi, Pwani kucheza na Ruvu Shooting na kuibuka na
ushindi wa mabao 3-0. Mwaikimba, Himid Mao ambaye alifunga kwa mara ya
kwanza, na Kipre walikuwa wafungaji wa mchezo huo. WAkaifunga JKT Mgambo kwa
mabao 2-0 kinda Farid Mussa alifunga bao lake la kwanza na kuungana na
Kimwaga, na Friday kisha Kipre alifunga bao lake la 12 la msimu.
Azam FC waliichapa Mbeya City katika
uwanja wa Sokoine, Mbeya kwa mabao 2-1 na kujihakikishia taji la kwanza la
ligi kuu baada ya miaka sita. Bocco alifunga bao la ushindi wakati matokeo
yakiwa sare ya bao 1-1 na kuipatia ubingwa klabu yake. Walimaliza msimu kwa
ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Ruvu. Kipre Tcheche alifunga bao lake la 13
la msimu na kuwa mfungaji bora wa klabu, Joseph Kimwaga na Mcha kila mmoja
alifunga mara moja.
' YOSSO WALIWABEBA '. Joseph Kimwaga, alifunga bao la ushindi wakati timu yake ya Azam ilipopata ushindi wa kushangaza dhidi ya waliokuwa watetezi wa taji, Yanga. Matokeo yakiwa sare ya magoli 2-2. Kimwaga kinda wa timu ya pili alimalizia pasi ya Kipre Tcheche katika dakika ya mwisho, mwezi septemba, mwaka uliopita. KELVIN FRED, kinda wa timu ya Taifa ya Vijana, Ngongoro Heroes, na timu ya Taifa ya Tanzania, alifunga goli la kusawazisha dakika tano kabla ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Yanga, 19 machi na kuisaidia timu yake iliyokuwa pungufu kwa zaidi ya dakika 25 kupata sare ya bao 1-1 na kulinda uongozi wao wa pointi saba dhidi ya Yanga. Michezo hii miwili ndiyo iliyoamua bingwa, na Azam walifanikiwa kupata pointi nne dhidi ya Yanga, ambao waliifunga Azam katika michezo yote miwili msimu uliopita wakati walipotwaa ubingwa. Pointi sita walizopata Azam dhidi ya Simba zimekuwa changamoto kubwa kwa Yanga ambao wameshindwa kuwafunga mahasimu wao hao msimu huu. Kupata pointi kumi dhidi ya Simba na Yanga, na nyingine nne dhidi ya Mbeya City. kumewasaidia sana timu hiyo iliyoanzishwa mwaka 2007. KOCHA, OMOG... Akiwa tayari mshindi wa taji la kombe la Shirikisho Afrika, kocha Mcameroon, Patrick Omog alitua, Azam akitokea kwa mabingwa wa Congo Brazzaville, AFC Leopard. Ameiongoza. Azam katika michezo 14 hadi sasa. Amepoteza mchezo mmoja tu, wakati Azam ilipofungwa na kutolewa na Ferreviaro Beira ya Msumbiji katika kombe la Shirikisho, ameiongoza timu yake kupata ushindi mara 11, huku mara kumi akifanya hivyo katika ligi kuu Tanzania Bara. Azam chini ya Omog imetoa sare mara mbili tu katika michezo 13 ya mzunguko wa pili katika ligi kuu.
KUFUNGA MABAO NA KUZUHIA. Azam
ilfunga magoli 53 na kuruhusu mabao 15 tu katika michezo 26 waliyocheza msimu
uliopita. Azam walikuwa na ngome imara, viungo wazuri, na washambuliaji
wakali kwa msimu mzima. Ukitoa timu ya Yanga ambayo imefunga magoli 59,
magoli nane zaidi ya Azam walikuwa tiimu liyokamilika kila idara.
Timu ya mwisho nje ya klabu za Yanga na Simba ni Mtibwa Sugar ya Morogoro. Mtibwa walitwaa mfululizo ubingwa huo katika miaka ya 1999, na 2000. Timu nyingine ziliwahi kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara, ni Coastal Union ya Tanga, 1988, Tukuyu Stars ya Mbeya, 1986, Pan Africans ya Dar es Salaam, 1982, Mseto ya Morogoro, 1975, na Cosmopolitan ya DAr es Salaam, 1967. Yanga SC, wametwaa ubingwa mara 24, Simba mara 19. Mtibwa mara mbili, na timu nyingine zimetwaa mara moja moja. Hongera AZam kwa kuwa mabingwa wapya wa ligi kuu Tanzania Bara. |
0714 08 43 98
Chanzo:shaffihdauda.com
Chanzo:shaffihdauda.com
0 comments:
Post a Comment